Na Salesi
Malula
Hayawi hayawi
sasa yamekua ndivyo ilivyokuwa siku ya jumapili ya tarehe 15 December 2013
ndani ya kanisa la Mlima wa Mabadiliko(River Of Life) ambapo watumishi wa Bwana
Mchungaji David Lutumba na Mkewe Mary ambao wamemtumikia Mungu kwa muda wa
miaka mingi na kazi yao kuonekana hatimaye wamesimikwa rasmi kuwa Maaskofu wa
Kanisa la mlima wa mabadiliko Duniani.
Tukio la
kusimikwa rasmi kwa maaskofu hao vijana lilifanyika Kanisani kwao Toangoma
wilayani Temeke Jijini Dar es salaam ambapo maelfu ya waumini kutoka mikoa
mbalimbali ya Tanzania wakiwepo watumishi wa Mungu kutoka nchi za Burundi,Kongo
Zambia na Afrika ya kusini waliweza kuhudhuria sherehe hizo za kusimikwa kwa
Viongozi wao tukio ambalo walikuwa wameliandaa kwa muda mrefu.
Katika sherehe
hizo watu walionekana kufurahia sana tukio hilo hasa kutokana na kanisa lao
kuwa limejiendesha kwa muda mrefu lakini lilikuwa limekosa Askofu jambo ambalo
kwa sasa limefungua mlango kwa viongozi wao kuchapa kazi kwa bidii ili kazi ya
Mungu isonge mbele na kukua zaidi ili maaskofu wengi waweze kusimikwa na
kiongozi wao Mkuu ndani na Nje ya Tanzania.
Kiongozi
Mkuu wa Kanisa la Hour Of Revival Askofu David Mathebula Kutoka Afrika ya
Kusini Ndiye aliyeongoza shughuli nzima ya kuwasimika Mtume Mary na Mumewe
David Lutumba maaskofu na viongozi wakuu wa kanisa la Mlima wa Mabadiliko
Duniani.
Lutumba na
Mkewe Mary ndio waanzilishi wa Kanisa la Mlima wa Mabadiliko kazi ambayo
waliianza kwa ugumu ambapo hawakuwa na Fedha wala dhahabu zaidi ya kuwa na Yes tu
aliyewawezesha kuisimamisha Kazi ya Mungu hadi hivi leo ambapo Mungu amewainua
na kuwafanikisha kuwa na kanisa kubwa lililojengwa kisasa na lenye waumini
zaidi ya elfu moja.
Makao makuu
ya Kanisa la Mlima wa mabadiliko kwa Neema ya Mungu yapo Tanzania na kwa muda
mfupi kanisa limefanikiwa kufungua
matawi mbalimbali katika maeneo ya Tabata Bima,Toangoma,Kibaha,na Morogoro kwa
hapa nchini ambapo yote yanaendelea vyema,na Nje ya Tanzania Mungu amewasaidia kufungua matawi nchini
Burundi,Congo ,Zambia na mipango inaendelea kufungua tawi nchini Uingereza hii
ni kwa Mujibu wa Askofu David Lutumba ambaye
alifanya mahojiano maalumu na gazeti la jibu mara baada ya kuimikwa
rasmi.
Akieleza
Historia ya Kanisa lake Askofu Lutumba alisema lilianza rasmi mwaka 2004 katika
ukumbi wa anatoglo uliopo Mnazi mmoja wakiwa na waumi 15 ambapo walidumu katika
ukumbi huo kwa muda wa miaka miwili na nusu ambapo walishindwa kulipa kodi ya
shilingi elfu 20 kutokana na waumini waliokuwa nao kutokuwa na uwezo wa kulipa
pango la mahali pa kuabudia hivyo ilibidi wahamie tabata nyumbani kwa mtu.
Hali ilikuwa
mbaya zaidi kwani waumini walipungua na kuwa 7 kwani wengi walishindwa kumudu
gharama za kufika tabata na kuamua kujiunga na madhehebu mengine yaliyo jirani.
Hatukukata tama
tuliendelea na ibada zetu kama kawaida bila kujali idadi ya watu na kwa neema
ya Mungu watu walianza kuongezeka ndio tukaamua sasa kutoka sebuleni na kuanza
kukodisha ukumbi ambapo Mungu aliusaidia kanisa likakua na kukua hali
iliyosababisha Neema kubwa ya kupata kiwanja chetu kikubwa na kufanikiwa
kujenga Kanisa kubwa pamoja na Ofisi mbalimbali zikiwepo studio hivyo mpaka
nasimikwa rasmi kua askofu kwakweli mimi na mke wangu tumetoka mbali sifa na
utukufu tunampa Bwana anayetuwezesha.
Akiongea katika
sherehe hizo Kabla ya kuwasimika Askofu Mathebula alisema Uaskofu ni jukumu
zito linalotakiwa kujitoa zaidi kwaajili yaw engine “hivyo ninapokwenda
kuwasimika siyo kwamba ninawapa cheo bali mnajitwika mzigo mkubwa zaidi wa
kuhakikisha mnalichunga na kuliangalia vyema kanisa la Bwana na kulifikisha
salama katika safari ya watu kwenda mbinguni hivyo nawapa changamoto nafasi hii
ninapowasimika manaanza kazi rasmi na mnatakiwa kuchapa kazi zaidi kuliko hapo
awali.
Mara baada
ya mahubiri Askofu Mathebula aliwaongoza kwa kiapo maalumu mbele ya madhabahu
ya Bwana na baadaye aliweza kuwapa Hati maalumu ya kiapo cha Uaskofu na mara
baada ya kuwasimika na kutangazwa rasmi kuwa sasa Kanisa la Mlima wa mabadiliko limepata maaskofu wa kuliongoza
Kanisa hilo.
Wakiongea kwa
unyenyekevu mara baada ya kusimikwa walilishukuru kanisa kwa maandalizi ya muda
mrefu,na walimshukuru Askofu Mathebula kwa moyo wake wa upendo uliomfanya aache
hata mazishi ya aliyekua Rais Mstaafu wa Taifa la Afrika ya kusini Mzee Nelson
Mandela na kututanguliza sisi hakika Baba Askofu Mathebula wewe ni Mtu wa Mungu
ambaye umetujali na kututhamini asante sana alisema Mtume na Askofu Mary
Lutumba kwa unyenyekevu huku Mathebula akionyesha kuguswa na shukrani hiyo kwa
kutikisa kichwa.
0 comments:
Post a Comment