VILIO na simanzi kubwa, jana viligubika katika mazishi ya mtoto mdogo, Teneli Malemi
Mang’ombe (11), aliyeuawa kwa kupigwa risasi na mwenyekiti wa zamani wa CCM Mkoa wa
Mwanza, Clement Mabina.
Mazishi hayo yalifanyika nyumbani kwa marehemu Kitongoji cha Kanyama, Kata ya Kisesa
wilayani Magu mkoani hapa.
Katika ibada ya mazishi hayo iliyoongozwa na Paroko wa Parokia ya Bujora Kisesa, Padri
Fabian Mhoja, akisaidiwa na Katekista wa Parokia hiyo, Faustine Lucas, ilihudhuriwa na
viongozi mbalimbali wa CCM na CHADEMA na serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya
Magu, Jacqueline Liana.
CCM washukuru kutotimuliwa msibani
Akitoa salamu za chama mara baada ya kumalizika maziko ya mtoto huyo aliyekuwa akisoma
darasa la sita Shule ya Msingi Kanyama, Katibu wa CCM Mkoa wa Mwanza, Joyce Masunga
alisema: “Tulishtushwa sana tuliposikia tukio hili. Lakini tunashukuru wazazi, ndugu na jamaa
hamjatufukuza kwenye msiba huu.”
Katibu huyo mbali na kutotoa rambirambi ya fedha, alijivunia chama chake kuandaa chakula
msibani hapo, na yeye kuosha mwili wa marehemu Taneli kwenye chumba cha kuhifadhia
marehemu hospitali ya Bugando.
“Kwa niaba ya chama tawala cha CCM, ninashukuru sana familia ya marehemu maana
hamjatufukuza katika msiba huu. Ingekuwa sehemu nyingine tungeweza kufukuzwa kwa sababu
kiongozi wa CCM amehusika kuua. Ila naomba sana tuweni na upendo, uvumilivu na amani,”
alisema Masunga huku akipiga magoti.
Mkuu wa wilaya hiyo, Jacqueline Liana alisema: “Kila mtu asimamie amani. Tukio kama hili
lisitokee tena katika wilaya yangu hii ya Magu, na ikiwezekana liwe la kwanza na la mwisho
kote nchini. Na Serikali ya Magu inatoa pole ya rambirambi kwa familia ya marehemu ya sh
300,000.”
Taneli aliuawa kwa kupigwa risasi na Mabina kisha nae kuuawa na wananchi papo hapo,
Desemba 15 mwaka huu, katika ugomvi wa mashamba kati yake na wananchi wa Kanyama.
Mazishi ya Mabina yawa gumzo
Wakati huo huo, Mabina ambaye alikuwa diwani wa Kata ya Kisesa wilayani Magu na mjumbe
wa mkutano mkuu wa taifa CCM aliyeuawa na wananchi wenye hasira, anatarajiwa kuzikwa
kesho, ambapo mazishi yake yatagharimu sh milioni 22.
Tetesi zilizopatikana kutoka kwa baadhi ya waombolezaji nyumbani kwa marehemu Mabina,
zinaeleza kwamba, Rais Jakaya Kikwete huenda akaongoza mazishi ya kiongozi huyo.
Baadhi ya wananchi wa Kisesa walionekana kufurahi kuuawa kwa kiongozi huyo, kwa madai
kwamba alikuwa amewasumbua kwa kuwadhulumu mashamba kwa muda mrefu.
MABINA AZIKWA KESHO
Jitokezedirectory
Thursday, December 19, 2013
Popular Posts
-
WIZARA ya Nishati na Madini, imesema tatizo la umeme nchini linatokana na kuchoka kwa miundombinu na hivyo kuzidiwa nguvu. Kauli hiyo ...
-
What to do in Zanzibar when you’re a tourist? I had booked myself a 4-day trip to the island, and, taking the advice of friends and a quic...
-
SERIKALI itatoa leseni kwa wafanyabiashara wa hapa nchini, ili kuwawezesha kuagiza tani 120,000 za sukari kutoka nje ya nchi na sukari hiyo...
-
Rap icon Tupac Shakur covers the latest issue of XXL in a profile that celebrates the rapper, who passed away 15 years ago. In the latest...
-
BAADHI ya wananchi wa Ubungo katika Manispaa ya Kinondoni, jana wavamia Ofisi za Kampuni inayosambaza maji katika Jiji la Dar es Salaam na...
-
WAMILIKI wa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans jana walitoka mahakamani kwa furaha baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutupilia mba...
-
Chimbuko la uvujaji wa mitihani nchini Tanzania lina historia ndefu inayoenda sambamba na kuundwa kwa BARAZA LA MITIHANI LA TAI...
-
RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amewapandisha vyeo maofisa wa juu wa jeshi pamoja na kuwahamisha baadhi ya maofisa akiwemo mlinzi wake mk...
-
I: UTANGULIZI a) Masuala ya Jumla Mheshimiwa Spika, 1. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi M...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK.Jakaya kikwete akilihutubia bunge mjini Dodoma.kulia ni spika wa Bunge Anne Makinda. Wab...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)



0 comments:
Post a Comment