MIONZI ya simu za mkononi inaweza kuathiri maendeleo ya ubongo wa watoto walioko tumboni mwa mama zao, utafiti umeeleza.Utafiti huo umetaja madhara mengine ya mionzi ya simu za mkononi kuwa ni uharibifu wa manii, mimba, kupungua kwa nguvu za kiume, kupoteza kumbukumbu na kuzaa watoto watukutu. Pia umeeleza kuwa matumizi kupita kiasi ya simu hizo, husababisha mtindio wa ubongo na upungufu wa udadisi kwa watoto tangu udogo wao. Hata hivyo, utafiti huo uliofanywa na Shule ya Tiba na Dawa ya Chuo Kikuu cha Yale, Marekani na kuripotiwa na Gazeti la The Telegraph la Uingereza, umepingwa na watafiti wengine, wakisema haujakidhi baadhi ya vigezo ili kuuthibitisha. Kiongozi wa jopo la utafiti huo, Profesa Hugh Taylor alisema utafiti huo ulioanzia kwa panya, baadaye ulithibitika kwa binadamu. Profesa Taylor ambaye pia ni Mkuu wa Idara ya Uzazi, Magonjwa ya Wanawake na Sayansi ya Uzazi, alisema: “Tulikuwa na panya wenye mimba katika maboksi na tuliwawekea simu juu ya vichwa vyao. Panya tuliokuwa tumewaweka katika bwawa lile, nusu yao walikuwa wazima na nusu yao walikufa. Panya waliokuwa hai tuliwaacha wajifungue na baada ya kujifungua, tukaanza kutafiti watoto wao.” “Panya ambao hawakuwa karibu na simu za mikononi walionekana kuwa werevu. Kumbukumbu zao hazikupungua ikilinganishwa na panya walioathiriwa na mionzi ya simu za mikononi ambao katika vipimo vya awali wakiwa tumboni, walionekana kuhangaika.” “Panya hao wenye mimba waliowekwa kwa siku 17 katika boksi hilo na simu kupigwa mfululizo juu ya vichwa vyao, walizaa watoto watukutu na waliokosa kumbukumbu.” Aliongeza: “Matokeo hayo yanaweza kutokea kwa binadamu pia. Mjamzito anayetumia simu ya mkononi muda mwingi, anaweza pia kuzaa taahira.”
Popular Posts
-
What to do in Zanzibar when you’re a tourist? I had booked myself a 4-day trip to the island, and, taking the advice of friends and a quic...
-
RAIS Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wakuu kutoka cheo cha Meja Jenerali kuwa Luteni Jenerali kuanzia Novemba 21,mwaka huu. K...
-
KUTOKANA na kile kichoonekana ni kutaka kukabiliana na uhaba wa sukari na kupanda kwa bei yake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajia kukuta...
-
Na Heka Paul na Shakila Galus- MAELEZO- Dar es salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuf...
-
MBUNGE wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu Sugu, ameungana na wananchi wanaotaka Katiba Mpya ifute uwepo wa wakuu wa wilaya...
-
Brazil's government has said it will implement 50bn reais ($30bn; £19bn) of spending cuts in order to curb inflation and help prevent t...
-
The rankings of Africa’s top higher education institutions is provided by the 4 International Colleges & Universities (4icu). ...
-
Katika Teknolojia Wiki Hii - Polisi yawasaka watumiaji Blackberry, wadukuzi walenga Blackberry, mashine za kupaa zilizotengenezwa nyumbani ...
-
WAMILIKI wa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans jana walitoka mahakamani kwa furaha baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutupilia mba...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)
0 comments:
Post a Comment