Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itafanya kila juhudi kuhakikisha kwamba maharibiko ya kuanguka sehemu ya jengo la Makumbusho ya Taifa Beit El Ajab yanarekebishwa na matengenezo ya jumla ya jengo hilo na majengo yote ya kihistoria yanasimamiwa ipasavyo. Akizungumza na waandishi wa habari katika makumbusho ya Mnazimmoja, Waziri Mbarouk amesema kutokana na heshima na hadhi ya jengo la Beit El Ajab kwa historia ya Zanzibar, kuanguka kwa jengo hilo kumeathiri shughuli za utalii kwani ni miongoni mwa vivutio vikuu vya Utalii ZANZIBAR. “Asilimia 70 ya wageni wanaotembelea sehemu za kihistoria huwa wanafika makumbusho ya Beit El Ajab’’, alisema Waziri Said Ali Mbarouk. Amesema uamuzi wa kuyahifadhi maeneo ya Historia ikiwemo jengo la Beit El Ajab utaendelea kupewa umuhimu mkubwa kwani ni sehemu ya urithi wa Utamaduni wa Zanzibar na yanahitaji kudumu kwa miaka mingi zaidi. “Jengo hili lililojengwa mwaka 1883 na Mfalme Barghash bin Said ni moja kati ya majengo yenye hadhi kubwa kihistoria, kijamii, kiuchumi na kisiasa kwa Zanzibar” alisisitiza Waziri Mbarouk. Amesema umaarufu wa jengo la Beit El Ajab unatokana na kuwa ni la kwanza Zanzibar kuwekewa huduma za kijamii kama vile umeme, simu, lifti na maji ya mfereji kabla ya huduma hizo hazijaanzishwa kwenye nchi nyingi za Afrika Mashariki. Ameongeza kuwa kutokana na maharibiko yaliyotokea Mamlaka ya Uhifadhi na Uendelezaji wa Mji Mkongwe inachukua hatua ya kuiarifu UNESCO kuhusu tukio hilo na kuomba msaada wa kitaalamu na fedha kulinusuru. Aidha amesema Idara ya Makumbusho na Mambo ya kale inafanya mawasiliano na watalaalamu wa majengo ya kale ili kupata tathmini ya hali ya jengo hilo na Kasri ya Kifalme na aina ya matengenezo ya kudumu na gharama zinazohitajika. Jengo la Makumbusho kuu ya Jumba la Ajab lilianguka usiku wa Jumamosi iliyopita wakati likiendelea kufanyiwa matengenezo na MACEMP na limewahi kutumika kwa sherehe na shughuli za utawala wakati wa ufalme, Makumbusho ya Chama cha ASP, Chuo cha Itikadi ya Chama na kuanzia mwaka 2002 likapewa hadhi ya kuwa makumbusho inayohusu Utamaduni wa Mswahili na Historia ya Zanzibar.
Popular Posts
-
What to do in Zanzibar when you’re a tourist? I had booked myself a 4-day trip to the island, and, taking the advice of friends and a quic...
-
MKUTANO MKUU TASWA DESEMBA 21 NA 22 Kiromo, BAGAMOYO
-
Takribani watu 24 wamekufa baada baada ya maporomoko yanayotokana na mvua za masika kutokea mashariki mwa Ugadna, wafanyakazi wa Shirika la...
-
Sheikh Mkuu wa Bakwata, Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kushoto), akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki katika Ma...
-
Newcastle imetoka sare ya 0-0 na Arsenal katika mchezo uliokuwa na kasoro za hapa na pale. Katika mchezo huo mshambuliaji wa Arsenal kuto...
-
The company behind Blackberry phones, Research In Motion (RIM) unveiled two new Blackberry Bold smartphones today as well as a new Blackber...
-
RAIS Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wakuu kutoka cheo cha Meja Jenerali kuwa Luteni Jenerali kuanzia Novemba 21,mwaka huu. K...
-
MTUNZI na mwigizaji wa filamu za Swahiliwood, Omary Clayton 'Ommy' ,amesisitiza kuwa yeye ndiye mwandishi wa filamu ya Shakira il...
-
On Monday, fans got their first look at Jay-Z and Kanye West’s new collaboration album, “Watch the Throne.” However, another Kanye controv...
-
KUTOKANA na kile kichoonekana ni kutaka kukabiliana na uhaba wa sukari na kupanda kwa bei yake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajia kukuta...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)
0 comments:
Post a Comment