RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amewapandisha vyeo maofisa wa juu wa jeshi pamoja na kuwahamisha baadhi ya maofisa akiwemo mlinzi wake mkuu, Kanali Wilson Mbadi. Kutokana na mabadiliko hayo, Jeshi la Polisi limethibitisha mabadiliko Kanali Mbadi ambaye alikuwa mlinzi mkuu wa Rais Museveni kwa muda wa miaka minne na kuwa Kamanda wa divisheni ya nne. Mabadiliko hayo katika Serikali ya Museveni yamesababisha Kanali Muhanga Kayanja, kuwa Kamanda Mkuu wa Polisi ambapo Kamanda mkuu wa Uganda katika Mji wa Mogadishu nchini Somalia, Brigedia Paul Lokech, amepelekwa Russia kuwa mshauri wa kijeshi. Vile vile Rais huyo amemteua Kanali, Peter Elwelu kuwa kamanda katika divisheni ya tatu ambapo amechukua nafasi ya Brigedia Burundi Nyamunywanisa, ambaye amepelekwa nchini Marekani katika Mji wa Washington kuwa mshauri wa kijeshi.
Popular Posts
-
I: UTANGULIZI a) Masuala ya Jumla Mheshimiwa Spika, 1. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi M...
-
Mtaalamu kutoka Finland asaidia mikakati ya tehama
-
WIZARA ya Nishati na Madini, imesema tatizo la umeme nchini linatokana na kuchoka kwa miundombinu na hivyo kuzidiwa nguvu. Kauli hiyo ...
-
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma ya Bunge ya Hesbu za Mashirika ya Umma, Kabwe Zuberi Zitto, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma ...
-
NEW YORK, Marekani VIDEO iliyoonyweshwa mwishoni mwa wiki katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ambayo ilielezea madhara ya taratibu ana...
-
JOSEPH KABILA Ni kijana na anawakilisha mustakabali wa nchi," Ndivyo walivyosema wafuasi wa Joseph Kabila wakati akiwasilisha fomu ...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)
0 comments:
Post a Comment