NEW YORK, Marekani VIDEO iliyoonyweshwa mwishoni mwa wiki katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ambayo ilielezea madhara ya taratibu anayoyapata mwanamke aliyeongeza ukubwa wa makalio, kwa dawa za silkoni imewashtua wanawake wengi waliowahi kutumia aina yoyote ya madawa hayo. Taarifa hiyo ilieleza kuwa madawa hayo badala ya kumfanya mwanamke awe laini, video hiyo inaelezea namna ukuaji wa haraka wa makalio pamoja na kuathirika huku yakiachwa katika sura mbaya sehemu za nyuma (chini) baada ya muda mfupi. Imebainika kuwa pamoja na dawa za kuongeza ukubwa wa makalio ya akina dada kupendwa, dawa hizo pia zina madhara kwa afya ya binadamu. Wataalamu wa mambo wanadai kwamba pamoja na kuongeza ukubwa wa makalio pia dawa huleta matatizo ya kuvimba kwa ngozi ya makalio katika mpangilio usio sahihi. Dawa hizo pia zimetajwa kuwa husababisha kwa uwepo mkubwa wa ugonjwa wa saratani. Video hiyo ya sekunde 20, inamwonyesha mwanamke aliyeongeza makalio yake kwa dawa za silicone akionyesha namna alivyoathirika kutokana na matumizi ya madawa hayo huku akisema : "Hivi ndivyo nilivyoongeza ukubwa wa makalio yangu". Anaongeza: "Sidhani kama ni sahihi kufanya hivi. Nadhani kuna ulazima wa kuyaondoa haya makalio yangu yote kwa sasa." alisikika akisema. Mpaka kufikia jana video hiyo ambayo pia iliwekwa katika mtandao wa kijamii wa Facebook tayari ulikuwa umependezwa na watu 278,000 wanaotembelea huku ikiwa imehamishwa na watu zaidi ya 430,000 wakipeleka katika kurasa zao. Mtumiaji mmoja wa mtandao huo kutoka nchini Marekani Donna Wright-Levy, alichangia akisema: "Mimi hupendelea kwenda maeneo kadhaa ambako hutengenezwa shepu yangu kwa madawa haya sasa nina ulazima wa kwenda kupima saratani". Ni vigumu kuthibitisha mwanamke huyu alitumia kliniki gani wakati alipofanyiwa uongezwaji wa ukubwa wa makalio yake miaka miwili iliyopita. Lakini mmoja wa madaktari kutoka kliniki ya upasuaji ya BAAPS Aurora nchini Uingereza Adrian Richards, ambaye pia ni mshauri wa upasuaji anaamini kuwa mwanamke huyo alifanyiwa marekebisho ya makalio yake kwa dawa za silicone. Alisema tatizo hutokea wakati nyama ya makalio inaposhindwa kuulinda vema mwili na kuwa imara katika nyama na mifupa na hivyo madhara huanza kutokea juu ya ngozi na kusambaa mpaka ndani ya nyama na baadaye mfupa. Ni matatizo ambayo ni ya kawaida kumfika mtumiaji ya dawa za kuongeza ukubwa wa maumbile iwe ni matiti ay makalio. Ni lazima itokee baada ya muda maana kama kitu kilipulizwa na upepo ina maana wakati wake ukiisha kitarudi kama awali. "Huyu mwanamke aliyaongeza makalio yake kwa nyuma na kwa juu zaidi hivyo tayari madhara yake yamekuwa ni makubwa kwa maana hakufanya upasuaji bali alitumia njia za mkato za silicone, " alisema Richards.
Popular Posts
-
WIZARA ya Nishati na Madini, imesema tatizo la umeme nchini linatokana na kuchoka kwa miundombinu na hivyo kuzidiwa nguvu. Kauli hiyo ...
-
What to do in Zanzibar when you’re a tourist? I had booked myself a 4-day trip to the island, and, taking the advice of friends and a quic...
-
SERIKALI itatoa leseni kwa wafanyabiashara wa hapa nchini, ili kuwawezesha kuagiza tani 120,000 za sukari kutoka nje ya nchi na sukari hiyo...
-
Rap icon Tupac Shakur covers the latest issue of XXL in a profile that celebrates the rapper, who passed away 15 years ago. In the latest...
-
BAADHI ya wananchi wa Ubungo katika Manispaa ya Kinondoni, jana wavamia Ofisi za Kampuni inayosambaza maji katika Jiji la Dar es Salaam na...
-
WAMILIKI wa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans jana walitoka mahakamani kwa furaha baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutupilia mba...
-
Chimbuko la uvujaji wa mitihani nchini Tanzania lina historia ndefu inayoenda sambamba na kuundwa kwa BARAZA LA MITIHANI LA TAI...
-
RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amewapandisha vyeo maofisa wa juu wa jeshi pamoja na kuwahamisha baadhi ya maofisa akiwemo mlinzi wake mk...
-
I: UTANGULIZI a) Masuala ya Jumla Mheshimiwa Spika, 1. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi M...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK.Jakaya kikwete akilihutubia bunge mjini Dodoma.kulia ni spika wa Bunge Anne Makinda. Wab...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)




0 comments:
Post a Comment