RAIS Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wakuu kutoka cheo cha Meja Jenerali kuwa Luteni Jenerali kuanzia Novemba 21,mwaka huu. Kwa mujibu ya taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Habari na Uhusiano ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), inaeleza kuwa maofisa wakuu waliopandishwa cheo ni Meja Jenerali, Sylvester Chacha Ryoba ambaye ni Mkurugenzi wa Kitengo cha Maafa ofisi ya Waziri Mkuu kuwa Luteni Jenerali. Mwingine ni Meja Jenerali, Charles Lawrance Makakala ambaye ni Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Ulinzi. Rais Kikwete na Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Jenerali Davis Mwamunyange amewapongeza wakuu hao. Wakati huohuo, Rais Jakaya Kikwete kesho anatarajia kufanya ziara ya siku moja mjini Rufiji, licha ya mambo mengine atahutubia mkutano wa hadhara mjini Ikwiriri. Akizungumza jana kwenye Baraza la Madiwani, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, Leonard Rwegasira alisema Rais Kikwete atapokelewa mpakani mwa wilaya ya Kilwa na Rufiji, eneo la Malendego. Rwegasira alisema wananchi wa Rufiji wametakiwa kujitokeza kwa wingi kumpokea kiongozi huyo atakapoingia wilayani hapa ikiwa ni ziara yake ya kwanza tangu kumalizika kwa Uchaguzi Mwaka 2010. Hata hivyo, Rwegasira aliwataka madiwani kuwajulisha wananchi kushiriki kumpokea.
Popular Posts
-
I: UTANGULIZI a) Masuala ya Jumla Mheshimiwa Spika, 1. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi M...
-
Mtaalamu kutoka Finland asaidia mikakati ya tehama
-
WIZARA ya Nishati na Madini, imesema tatizo la umeme nchini linatokana na kuchoka kwa miundombinu na hivyo kuzidiwa nguvu. Kauli hiyo ...
-
NEW YORK, Marekani VIDEO iliyoonyweshwa mwishoni mwa wiki katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ambayo ilielezea madhara ya taratibu ana...
-
JOSEPH KABILA Ni kijana na anawakilisha mustakabali wa nchi," Ndivyo walivyosema wafuasi wa Joseph Kabila wakati akiwasilisha fomu ...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)
0 comments:
Post a Comment