LOS ANGELES, Marekani MWANAMUZIKI Mary Jane Blige ni kati ya wanamuziki mahiri wa Marekani.Blige, aliyezaliwa Januari 11, 1971, pia anasifika kutokana na kuwa prodyuza na kucheza filamu. Ameshinda tuzo tisa za Grammy na American Music Award kutokana na muziki wa R&B, Rap, Gospel na Pop. Blige alianza muziki mwaka 1992 baada ya kutoa albamu ya kwanza aliyoipa jina la 'What's the 411'. Mwanamuziki huyo ameuza zaidi ya nakala milioni 50 za albamu za muziki sehemu mbalimbali duniani. Anahesabiwa kuwa miongoni mwa wanamuziki wa R&B wenye mafanikio zaidi katika kipindi cha miaka 25. Blige pia amejizolea sifa kubwa kutokana na kazi zake za filamu na manukato. Aling'ara katika filamu ya Tyler Perry iliyotolewa mwaka 2009. Mwanamuziki huyo anakadiriwa kuwa na utajiri wa kiasi cha Dola 45 milioni (Sh 70 bilioni). Mwaka 2004, alianzisha lebo ya Matriarch Records na amekuwa akisambaza kazi za wanamuziki mbalimbali. Pia anatengeneza manukato yanayoitwa My Life na My Life Blossom HSN. Blige pia ana kampuni ya kutengeneza miwani ya jua ya "Melodies by MJB". Pia anafanya shughuli za matangazo na kampuni za Reebok, Air Jordan, Pepsi, Coca-Cola, Gap, Target, American Express, AT&T Inc., M∑A∑C, Apple Inc., Burger King na Chevrolet. Mwanamuziki huyo anaishi Saddle River, New Jersey, Marekani na anamiliki jumba lenye thamani ya Dola 17 milioni (Sh 26 bilioni). Pia ana magari kibao yakiwamo Chevloret, Royce Royce Phantom, Ferrari na Range Rover.
Popular Posts
-
What to do in Zanzibar when you’re a tourist? I had booked myself a 4-day trip to the island, and, taking the advice of friends and a quic...
-
RAIS Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wakuu kutoka cheo cha Meja Jenerali kuwa Luteni Jenerali kuanzia Novemba 21,mwaka huu. K...
-
KUTOKANA na kile kichoonekana ni kutaka kukabiliana na uhaba wa sukari na kupanda kwa bei yake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajia kukuta...
-
Na Heka Paul na Shakila Galus- MAELEZO- Dar es salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuf...
-
MBUNGE wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu Sugu, ameungana na wananchi wanaotaka Katiba Mpya ifute uwepo wa wakuu wa wilaya...
-
Brazil's government has said it will implement 50bn reais ($30bn; £19bn) of spending cuts in order to curb inflation and help prevent t...
-
The rankings of Africa’s top higher education institutions is provided by the 4 International Colleges & Universities (4icu). ...
-
Katika Teknolojia Wiki Hii - Polisi yawasaka watumiaji Blackberry, wadukuzi walenga Blackberry, mashine za kupaa zilizotengenezwa nyumbani ...
-
WAMILIKI wa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans jana walitoka mahakamani kwa furaha baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutupilia mba...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)
0 comments:
Post a Comment