MWIGIZAJI Nyota katika tasnia ya filamu Swahiliwood, Yvonne Cherryl �Monalisa� amewashutumu wasanii wenzake kwa kusema uongo katika jamii kuhusu maisha yao halisi pamoja na malipo wanayopata. Binti huyo amedai kwa kufanya hivyo wasanii wengi wemejikuta katika maisha ya kuunga unga kutokana uongo huo. �Baadhi ya wasanii wa filamu wanadanganya sana kuhusu hali halisi ya maisha yao, mtu akipata nafasi ya kuongea na vyombo vya habari kuhusu malipo na maisha yake halisi utakuta akisema kuwa yeye bila kulipwa milioni tano hawezi kushiriki katika filamu, lakini ukweli hakuna msanii wa kawaida anayelipwa fedha kama hizo katika tasnia ya filamu Bongo mimi mwenyewe ni mtayarishaji,� anasema Monalisa. Anaendelea kudai kuwa kutokana na udanganyifu huo Serikali kupitia Bodi ya Filamu iliamua kuongeza gharama za kibali cha kurekodi filamu hadi kufikia Shilingi 500,000 jambo lilofanya wasanii walalamike kama ni fedha kubwa sana kulingana na malipo ya filamu, lakini ilitokana na udanganyifu kutoka kwa baadhi ya wasanii wa filamu kudanganya, mwanadada huyo anasema hali ya soko la filamu ni mbaya kwa sasa.
Popular Posts
-
I: UTANGULIZI a) Masuala ya Jumla Mheshimiwa Spika, 1. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi M...
-
Mtaalamu kutoka Finland asaidia mikakati ya tehama
-
WIZARA ya Nishati na Madini, imesema tatizo la umeme nchini linatokana na kuchoka kwa miundombinu na hivyo kuzidiwa nguvu. Kauli hiyo ...
-
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma ya Bunge ya Hesbu za Mashirika ya Umma, Kabwe Zuberi Zitto, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma ...
-
NEW YORK, Marekani VIDEO iliyoonyweshwa mwishoni mwa wiki katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ambayo ilielezea madhara ya taratibu ana...
-
JOSEPH KABILA Ni kijana na anawakilisha mustakabali wa nchi," Ndivyo walivyosema wafuasi wa Joseph Kabila wakati akiwasilisha fomu ...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)
0 comments:
Post a Comment