HERIETH MAKWETTA MSANII wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Rehema Chalamila maarufu kama Ray C, yupo katika kituo maalumu cha msaada wa kuacha matumizi ya dawa za kulevya akipatiwa matibabu. Kwa mujibu wa The Kenyan Daily Post, mwanamuziki huyo alikubali kupatiwa matibabu na ni miongoni mwa watu kadhaa wanaopata matibabu ya kuachana na ulevi wa dawa hizo. Anasifika kwa uzuri, sauti nyororo na wepesi wa kuzungusha kiuno jukwaani. Lakini leo hii, mwanamuzi huyo anakabiliwa na tatizo na usugu wa matumizi ya dawa za kulevya. Ray C ambaye alianza kuimba akiwa na umri mdogo, alitumia utoto wake akiishi jijini Dar es Salaam na Uganda. Alianza kujulikana kama DJ wa redio jijini Dar es Salaam katika stesheni ya Clouds FM. Alipata mafunzo ya sauti na kuanza kuimba mpaka alipotoa albamu yake ya kwanza 'Mapenzi Yangu' mwaka 2003. Albamu ilifanya vizuri nchini Tanzania, lakini aliendelea na muziki na kuzindua albamu nyingine mwaka 2004 'Na Wewe Milele' iliyovuka mipaka ya Tanzania na kusambaa Afrika Mashariki. Baada ya kufanya vizuri katika albamu yake ya pili, Ray C alibahatika kushinda tuzo ya Kilimanjaro na Kisima Music Awards na kuchukua nafasi kati ya wanamuziki wanaofanya vema Afrika Mashariki. Alizindua albamu yake ya tatu iliyopewa jina la 'Ray C' mwaka 2007. Albamu hiyo ilikuwa na mchanganyiko wa taarab na bongo fleva. Mbali na kumudu mitindo hiyo ya muziki, Ray C ni mkali wa Bhangra, RnB lakini sasa makali yake hayo yote yameishia kwenye kliniki akipewa mbinu za kuachana na dawa za kulevya. Tangu kutolewa kwa picha za utupu za mwanamuziki huyo anayecheza na kuimba ndipo umaarufu wake ulipoathiriwa na kushuka kwa kasi. Ray C amewahi kufanya kazi za kimataifa pamoja na kuonekana katika mataifa ya Uingereza, Marekani, Ujerumani, Sweden, China, Uganda, Nigeria, India, Afrika Kusini na Kenya. Hivi karibuni msanii huyo aliweka makazi yake nchini Kenya na muziki wake umekuwa maarufu baada ya kufanya kolabo ya wimbo wake 'Moto moto' akimshirikisha staa 'French Boy'. Akiwa nchini Kenya aliendelea kupata matatizo mengi ikiwa ni pamoja na shutuma dhidi ya promota Sadat Muhindi na kuibuka kwa mzozo kati yake na mhariri nchini Kenya, Charles Otieno. Katika ugomvi wake na promota Saadat Muhindi kwamba alikuwa akimlazimisha kufanya naye mapenzi kabla ya kufanya shoo nchini Sudan, Ray C alipofanya mahojiano na Hot Secrets, aliweka nayana kuwa Saadat alianza kuchanganya biashara ya muziki na mapenzi. Kutokana na hilo, promota huyo aliamua kuahirisha ziara ya muziki ndani ya Kenya na Sudan, ziara ambayo ingechukua siku 10. Ray C alisema Muhindi alianza kuonyesha tamaa ya mapenzi dhidi yake wakati alipotua jijini Dar es Salaam kufanya utafiti wa kinywaji chake kipya kiitwacho Dash. Kinywaji hicho hakina kilevi. Akizungumzia tuhuma hizo Saadat alisema: �Kama anayoyasema yana ukweli wowote ilikuwa akaamua kuja tena Kenya baada ya mimi kuondoka Dar es Salaam? Lakini pia tujiulize kwanini alikuja na rafiki yake wa kiume huku akijua kuwa mimi ni mwovu na hakuwahi kumweleza hilo? �Kwa taarifa yako niliwalipia wote wawili tiketi za ndege kuja jijini Nairobi. Kama ningekuwa na nia mbaya kamwe nisingekuwa na akili ya wendawazimu kama hiyo. Naamini ulikuwa mpango wa kuniharibia biashara zangu.� Kabla ya dosari hiyo, Saadat alikubaliana na Ray C awe balozi wa kinywaji chake cha Dash nchini Tanzania na kuzunguka katika miji ipatayo 10 kutangaza kinywaji hicho. Lakini kilichotokea baadaye ni kuwa wakati walipofanya shoo mjini Nakuru, wawili hao wakatangaza kuvunjwa kwa mkataba.
Popular Posts
-
JAJI Mkuu, Mohamed Chande Othman ameeleza sababu za kutokuwa kwenye jopo la majaji waliopangwa kusikiliza kesi ya aliyekuwa mbunge wa Cha...
-
KIASI cha fidia ambacho Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) liliamriwa na Mahakama Kuu Dar es Salaam, kuilipa Kampuni ya Kufua Umeme wa D...
-
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akiwaonyesha waandishi wa habari (Ha...
-
Wazungu wawili raia wa Ujerumani, VEIXLAR MARLM (24), WEIXLER ROLAND (21) wamenusurika kuuawa baada ya kutekwa na watu waliojifanya waendes...
-
Nyaraka zilizonekana katika jengo la serikali ya Libya mjini Tripoli, zinaonesha uhusiano wa karibu baina ya mashirika ya ujasusi ya mataif...
-
Sheikh Mkuu wa Bakwata, Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kushoto), akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki katika Ma...
-
safara wa magari wenye ulinzi na silaha kutoka Libya umevuka mpaka kuingia nchini Niger, ripoti zinasema. Msafara huo unaaminika ni wa w...
-
Mtaalamu kutoka Finland asaidia mikakati ya tehama
-
MBUNGE wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu Sugu, ameungana na wananchi wanaotaka Katiba Mpya ifute uwepo wa wakuu wa wilaya...
-
BAADA ya juzi Jeshi la Polisi kuwahoji na kuwaachulia huru wabunge wa Chadema, jana asubuhi walikamatwa na kutupwa korokoroni hadi kesho ...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)




0 comments:
Post a Comment