MTUNZI na mwigizaji wa filamu za Swahiliwood, Omary Clayton 'Ommy' ,amesisitiza kuwa yeye ndiye mwandishi wa filamu ya Shakira iliyoigizwa na kuandaliwa na mwigizaji nyota wa Bongo, Vincent Kigosi 'Ray'. Ommy ametamka hayo kufuatia utata uliojitokeza kuhusu filamu hiyo kwamba imeandikwa na Ali Yakuti. Ommy amedai kuwa muswada wa filamu ya Shakira alimkabidhi Ray ukiwa umekamilika kila kitu hivyo Ray badala ya kupokea yeye akamwambia ampatie Ali Yakuti aukague na kuruhusu utumike kwa sababu hadithi yake ilikuwa nzuri. �Ukweli mimi ndiye mwandishi wa muswada wa filamu ya Shakira, nakumbuka hata tulivyokutana katika mafunzo ya utayarishaji filamu na kaka Ali, alikiri kuwa mimi ndiye mwandishi," alisema. "Kukuthibitishia kuwa mimi ni mkali kuliko yeye, ulifanyika usaili na nilimpoteza vibaya hadi mimi kuchukuliwa na Wazungu. Kisanaa mimi bora kuliko yeye, kiumri yeye ni mkubwa, ninamheshimu ni kaka yangu." Mwanaspoti lilizungumza pia na Ali Yakuti naye alisema kuwa maneno ya mtunzi huyo amekuwa akiyasikia mara kwa mara, lakini kwa sababu ukweli upo wazi hana sababu ya kubishana na mtu anayetafuta umaarufu kupitia kazi za watu wengine. "Ommy alikuja na kusimulia wazo ambalo halikuwa limekamilika. Mimi ndiye niliyeandika muswada," alisema Yakuti.
Popular Posts
-
I: UTANGULIZI a) Masuala ya Jumla Mheshimiwa Spika, 1. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi M...
-
Mtaalamu kutoka Finland asaidia mikakati ya tehama
-
WIZARA ya Nishati na Madini, imesema tatizo la umeme nchini linatokana na kuchoka kwa miundombinu na hivyo kuzidiwa nguvu. Kauli hiyo ...
-
NEW YORK, Marekani VIDEO iliyoonyweshwa mwishoni mwa wiki katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ambayo ilielezea madhara ya taratibu ana...
-
JOSEPH KABILA Ni kijana na anawakilisha mustakabali wa nchi," Ndivyo walivyosema wafuasi wa Joseph Kabila wakati akiwasilisha fomu ...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)
0 comments:
Post a Comment