UJENZI wa Barabara ya Kilwa, jijini Dar es Salaam ambayo Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli alikataa kuipokea mwaka 2011, baada ya kujengwa chini ya kiwango, umekamilika.Ujenzi wa kipande hicho cha kilomita 5.1 kutoka Mtongani hadi Mbagala Rangi Tatu, ulikamilika jana baada ya magari kuruhusiwa kutumia barabara bila vikwazo vilivyokuwapo wakati wa ujenzi. Mafundi wa Kampuni ya Kajima waliokuwa wakijenga kipande hicho cha barabara, jana walionekana wakiwa katika hatua za mwisho za kusawazisha udongo katikati ya barabara hiyo yenye njia nne.Msongamano wa magari ulikuwa ukiwasababishia usumbufu watumiaji wa barabara hiyo inayounganisha Dar es Salaam na mikoa ya Lindi na Mtwara, sasa umekwisha. Magufuli alikataa kuipokea barabara hiyo kutoka katika Serikali ya Japan, iliyotoa msaada wa fedha na ujenzi kufanywa na Kampuni ya Kajima, baada ya kujiridhisha kuwa ilijengwa chini ya kiwango. Magufuli alimweleza Balozi wa Japan nchini, Masaki Okada kwamba asingeipokea barabara iliyo chini ya kiwango hata kama imetolewa kama msaada kwa Tanzania. Baada ya msimamo huo wa Serikali, Japan ilifanya uchunguzi na kubaini kuwa kampuni hiyo ilijenga barabara hiyo chini ya kiwango. Kutokana na hali hiyo, Balozi Okada aliahidi kurudia ujenzi wa kilometa 5.1 kipande ambacho waligundua kuwa kampuni hiyo ilijenga chini ya kiwango.Kazi ya ujenzi huo ilianza Juni mwaka huu. Baada ya kauli hiyo ya Balozi, Dk Magufuli alimtaka mkandarasi huyo kuondoa tabaka la lami na kuweka tabaka jingine gumu lenye sentimita saba jambo ambalo limetekelezwa baada ya marudio.Ujenzi wa Barabara ya Kilwa yenye urefu wa kilomita 13.5 kutoka bandarini hadi Mbagala Rangitatu ulizinduliwa kwa kuwekwa jiwe la msingi na Rais Jakaya Kikwete mwaka 2007.
Popular Posts
-
MKUTANO MKUU TASWA DESEMBA 21 NA 22 Kiromo, BAGAMOYO
-
Takribani watu 24 wamekufa baada baada ya maporomoko yanayotokana na mvua za masika kutokea mashariki mwa Ugadna, wafanyakazi wa Shirika la...
-
What to do in Zanzibar when you’re a tourist? I had booked myself a 4-day trip to the island, and, taking the advice of friends and a quic...
-
Newcastle imetoka sare ya 0-0 na Arsenal katika mchezo uliokuwa na kasoro za hapa na pale. Katika mchezo huo mshambuliaji wa Arsenal kuto...
-
The company behind Blackberry phones, Research In Motion (RIM) unveiled two new Blackberry Bold smartphones today as well as a new Blackber...
-
RAIS Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wakuu kutoka cheo cha Meja Jenerali kuwa Luteni Jenerali kuanzia Novemba 21,mwaka huu. K...
-
MTUNZI na mwigizaji wa filamu za Swahiliwood, Omary Clayton 'Ommy' ,amesisitiza kuwa yeye ndiye mwandishi wa filamu ya Shakira il...
-
On Monday, fans got their first look at Jay-Z and Kanye West’s new collaboration album, “Watch the Throne.” However, another Kanye controv...
-
KUTOKANA na kile kichoonekana ni kutaka kukabiliana na uhaba wa sukari na kupanda kwa bei yake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajia kukuta...
-
Mwezi huu, Majimbo mawili nchini marekani yamepiga kura kuhalalisha , kudhibiti na kutoza kodi bangi. Kutokana na matangazo ya k...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)
0 comments:
Post a Comment