Wanasiasa wawili wa Kenya wanaotaraji kugombea uongozi na ambao wameshtakiwa na Mahakama ya Uhalifu ya Kimataifa, ICC, kwa kuchochea fujo baada ya uchaguzi, wametangaza rasmi kuwa wanaungana katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, Katika mkutano wa hadhara uliofanywa mjini Nakuru makamo wa Waziri Mkuu, Uhuru Kenyatta, alisema atagombea urais na waziri wa zamani, William Ruto, alisema yeye atakuwa mgombea mwenza wa Bwana Kenyatta. Siku ya Ijumaa shirika la Kenya la kutetea haki (the International Centre for Peace and Conflict) lilifikisha kesi mahakama makuu kudai kuwa wanasiasa hao hawafai kushika madaraka. Wanasiasa wengine maarufu wa Kenya piya wameshtakiwa na ICC.
Popular Posts
-
I: UTANGULIZI a) Masuala ya Jumla Mheshimiwa Spika, 1. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi M...
-
Mtaalamu kutoka Finland asaidia mikakati ya tehama
-
WIZARA ya Nishati na Madini, imesema tatizo la umeme nchini linatokana na kuchoka kwa miundombinu na hivyo kuzidiwa nguvu. Kauli hiyo ...
-
NEW YORK, Marekani VIDEO iliyoonyweshwa mwishoni mwa wiki katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ambayo ilielezea madhara ya taratibu ana...
-
JOSEPH KABILA Ni kijana na anawakilisha mustakabali wa nchi," Ndivyo walivyosema wafuasi wa Joseph Kabila wakati akiwasilisha fomu ...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)
0 comments:
Post a Comment