MBUNGE wa Ubungo (Chadema), John Mnyika amesema ataongeza nguvu ya wabunge wanaotaka Serikali kuchukua hatua za haraka kuwataja baadhi ya viongozi na wafanyabiashara wanaodaiwa kuficha nje mabilioni ya fedha yanayosadikiwa kupatikana kwa njia isiyo sahihi. Mnyika aliyasema hayo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika Kata ya Saranga Mbezi jijini Dar es Salaam, ambapo tayari Mbunge wa jimbo la Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe alishatoa kauli kama hiyo ya kuitaka Serikali kuchukua hatua za haraka kuwataja watu hao kabla ya vikao vya Bunge vya mwezi Aprili. Akizungumza katika mkutano huo, Mnyika alisema Serikali itegemee kupata upinzani mkubwa katika vikao vya Bunge Aprili mwakani kama haita jisafisha kwa kuwataja watu hao na kuwachukulia hatua. “Nia yetu ni kuhakikisha watu wote wanaodaiwa kuwa na akaunti mbalimbali nje ya nchi Serikali inawachukulia hatua pamoja na kuwataja kwa majina ili watanzania waeze kuwafahamu watu wanao wasababisha waishi katika hali ngumu,” alisema Mnyika na kuongeza: “Nijambo la kushangaza kusikia kwamba Serikali ya CCM inasema wapinzani ndiyo tuwataje lakini suala hilo lipo wazi kwani kama itakumbukwa, Septemba 15 mwaka 2010 katika viwanja vya Mwembeyanga tulitaja majina hayo na wengine kwa sasa ndio Viongozi wakubwa ndani ya Bunge.” Mnyika alibainisha kwamba Chadema itaendelea na kasi yake ile ile hadi kuhakikisha viongozi wote wanaodaiwa kuwa na akaunti nje ya nchi wanajulikana wazi ili Watanzania wawafahamu watu wanao tumia kodi zao kwa masilahi yao binafsi. Katika hatua nyingine, Mnyika alisema suala la usafiri katika jiji la Dar es Salaam bado ni tatizo kwani hata kuwapo kwa usafiri wa treni sio suluhisho kutokana na Serikali kupata hasara ya Sh10 milioni kila baada ya siku tano kutokana na undeshaji wa usafiri huo. Alisema kutokana na maandalizi duni Serikali inapata hasara ya Sh10 milioni jambo ambalo ni hatari kwani itafikia hatua usafiri huo wa Treni utasimama. “Ni vyema Serikali ikajipanga vizuri kwani kwa sasa wakazi wengi wa Jiji la Dar es Salaam wanafurahia usafiri wa Treni lakini ipo siku usafiri huo utasimama kutokana na kuendeshwa kwa hasara kubwa,” alisema na kuongeza; “Jambo hilo linatokana na kuwa na miundombinu mibovu na maandalizi duni yaliyofanywa na mawaziri wa uchukuzi waliopita.”
Popular Posts
-
WIZARA ya Nishati na Madini, imesema tatizo la umeme nchini linatokana na kuchoka kwa miundombinu na hivyo kuzidiwa nguvu. Kauli hiyo ...
-
What to do in Zanzibar when you’re a tourist? I had booked myself a 4-day trip to the island, and, taking the advice of friends and a quic...
-
SERIKALI itatoa leseni kwa wafanyabiashara wa hapa nchini, ili kuwawezesha kuagiza tani 120,000 za sukari kutoka nje ya nchi na sukari hiyo...
-
Rap icon Tupac Shakur covers the latest issue of XXL in a profile that celebrates the rapper, who passed away 15 years ago. In the latest...
-
BAADHI ya wananchi wa Ubungo katika Manispaa ya Kinondoni, jana wavamia Ofisi za Kampuni inayosambaza maji katika Jiji la Dar es Salaam na...
-
WAMILIKI wa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans jana walitoka mahakamani kwa furaha baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutupilia mba...
-
Chimbuko la uvujaji wa mitihani nchini Tanzania lina historia ndefu inayoenda sambamba na kuundwa kwa BARAZA LA MITIHANI LA TAI...
-
RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amewapandisha vyeo maofisa wa juu wa jeshi pamoja na kuwahamisha baadhi ya maofisa akiwemo mlinzi wake mk...
-
I: UTANGULIZI a) Masuala ya Jumla Mheshimiwa Spika, 1. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi M...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK.Jakaya kikwete akilihutubia bunge mjini Dodoma.kulia ni spika wa Bunge Anne Makinda. Wab...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)




0 comments:
Post a Comment