JAJI MKUU AELEZA SABABU ZA KUJITOA KESI YA LEMA
JAJI Mkuu, Mohamed Chande Othman ameeleza sababu za kutokuwa kwenye jopo la majaji waliopangwa kusikiliza kesi ya aliyekuwa mbunge wa Chadema mkoani Arusha, Godbless Lema. Jaji mkuu, alitoa maelezo haya jana alipozungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu kwenye mahafali ya 12 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA). “Ngoja nitolee ufafanuzi suala hilo ili jamii itambue utaratibu wa uendeshaji wa Mahakama ya Rufani, ambayo ina majaji 16 nchini,” alisema Jaji Othman. Jaji Othman alisema kimsingi hajajitoa kushughulikia kesi hiyo, ila siku ambayo kesi hiyo inatajwa, atakuwa nchini India kuhudhuria Mkutano Mkuu wa 13 wa Majaji Wakuu Duniani. Maelezo hayo ya Jaji Chande yamekuja siku tatu baada ya gazeti hili kuripoti kuwa, mkuu huyo wa mhimili wa Mahakama nchini amejitoa kusikiliza kesi hiyo na nafasi yake imechukuliwa na Jaji Bernard Luanda. “Kwanza ifahamike kwamba, jaji wa Mahakama ya rufani hana ubia na kesi yoyote kwa mujibu wa utaratibu. Jaji yeyote kati ya majaji 16 wa mahakama ya rufani nchini ana mamlaka ya kusikiliza kesi yoyote ya rufani,” alieleza Jaji Othman. Jaji Othman alifafanua kuwa, rufani ya Lema ni miongoni mwa kesi tatu za uchaguzi zilizobaki ambazo kwa mujibu wa taratibu za kisheria, huanza kusikilizwa baada ya muda wa mwaka mmoja na hukumu yake ni lazima itolewe ndani ya mwaka mmoja tangu kuanza kwake. “Hivyo basi, kwa vile Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufaa anaweza kuisikiliza kesi hiyo, hakukuwa na sababu inisubiri mimi,” alisema. Jaji Othman alitaja kesi nyingine za uchaguzi zitakazoanza kufanyiwa vikao vya rufani na jopo la majaji wa Mahakama ya Rufani kuwa, ni ile ya Jimbo la Ubungo kati ya Hawa Ng’umbi na John Mnyika ambayo itakuwa chini ya jopo la majaji watatu; Jaji Nathalia Kimaro, Jaji Salum, Salum Masati na Jaji Katherine Oriyo. Nyingine ni ya Jimbo la Ilemela ya Yusuph Yussuph Masengela Lupilya na wenzake wawili dhidi ya Highness Kiwia na wenzake wawili, ambayo itakuwa chini ya jopo la Majaji Januari Msofe, Jaji Beard Luanda na Jaji Salum Massati. Alisema rufani ya Lema haijaanza kusikilizwa kwa jaji yeyote, hivyo yeye asingeweza kujitoa kwa kuwa hajapangiwa. “Kinachotatiza hapa ni kwamba, watu wanaifungamanisha rufani hii na ile ya Arusha ambayo mimi nilikuwa miongoni mwa jopo la majaji kama mwenyekiti.Popular Posts
-
SERIKALI itatoa leseni kwa wafanyabiashara wa hapa nchini, ili kuwawezesha kuagiza tani 120,000 za sukari kutoka nje ya nchi na sukari hiyo...
-
Waziri wa Habari Utamaduni Utalii na Michezo Said Ali Mbarouk amesema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itafanya kila juhudi kuhakikisha...
-
Huduma ya Maji na Nishati (EWURA), Mhandisi Godwin Samwel, akizungumza na wanahabari jana jijini, Dar es Salaam kuhusu kupanda kwa bei za m...
-
WAZIRI wa Uchukuzi, Dk Harrison Mwakyembe amewapiga marufuku wafanyakazi wote walio chini ya wizara yake kusafiri kwa ndege katika daraja...
-
Dar es Salaam. Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka amesema mwezi ujao wanatarajia kutangaza kima cha chini cha mshahara kwa wafany...
-
JAJI MKUU AELEZA SABABU ZA KUJITOA KESI YA LEMA JAJI Mkuu, Mohamed Chande Othman ameeleza sababu za kutokuwa kwenye jopo la majaji wali...
-
Katika kuitikia kaulimbiu ya kilimo kwanza Kampuni ya Utalii ya Cordial Tours Yenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam imeamua kuunga Mk...
-
WAKATI mpango wa mwaka mmoja wa umeme wa dharura ukiwa umemalizika, utekelezaji wake umeshindwa kufikiwa na matokeo yake tatizo la mgaw...
-
UPELELEZI wa kesi inayomkabili Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, anayekabiliwa na kesi ya mauaji katika Maha...
-
AFRICA has made remarkable progress in fighting malaria under alliance championed by President Jakaya Kikwete, but the success was describe...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)
0 comments:
Post a Comment