Mahudhurio ya wajumbe yamkatisha tamaa Dk Slaa
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeeo( Chadema), Dk Willbrod Slaa jana alizungumzia kukatishwa kwake tamaa na mahudhurio ya wajumbe wa mkutano mkuu wa chama hicho Jimbo la Kinondoni jijini Dar es Salaam. Dk Slaa alisema hayo jana wakati wa Mkutano Mkuu wa jimbo hilo baada ya mahudhurio kuwa hafifu. Alisema asilimia 50 ya mahudhurio ya wajumbe katika jimbo hilo ni aibu na yanatia shaka iwapo wana nia ya dhati ya kushika dola mwaka 2015. “Dalili hii inaonyesha kwamba kuna tatizo, hivyo kupitia mkutano huu tutayamaliza na kurudisha ufanisi wa chama” alisema Dk Slaa na kuongeza: “Chadema ni chama ambacho kinajiandaa kushika dola mwaka 2015, endapo hali hii itaendelea ya wajumbe kutafutana kwa njia ya simu itakuwa hatari wakati wa kuunda baraza la mawaziri” alisema na kuongeza: “Haiwezekani Rais akawa anatafuta baraza la mawaziri kwa njia ya simu, kwani bila kujipanga wakati huu itakuwa ngumu huko mbele tunakokwenda,” alisema. Katika mazungumzo yake Dk Slaa alisema, wanakusudia kutoa tamko la nini ifanyike kuhusu mauaji mbalimbali ya wananchi yalifanywa na polisi baada ya Rais Jakaya Kikwete kushindwa kuwachukulia hatua Waziri wa Mambo ya Ndani , Dk Emmanuel Nchimbi, Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Saidi Mwema na Kamanda wa Mkoa wa Iringa Michael Kamhanda. “Hatuwezi kutulia huku tukiona vyombo ambavyo vinatakiwa kulinda usalama wa raia ndio vinakuwa vya kwanza kuwaua raia wasiokuwa na hatia huku kiongozi wa nchini (Rais Kikwete) akiwa kimya bila kutoa tamko lolote,” alisema. Katika mkutano huo, wajumbe walitakiwa kufika mapema kwa ajili ya kuanza kwa mkutano saa 4 hadi saa 6 mchana, lakini kutokana na ufinyu wa mahudhurio, mkutano huo ulianza saa 6.47 mchana. Sifa zimwendee Mwenyekiti wa Chama hicho Jimbo la Kinondoni, Deo Mushi ambaye alifanya kazi ya kuwatafuta wajumbe hao kwa njia ya simu ili kutimiza idadi ya asilimia 50. Mratibu wa Mkutano huo, Mkurungenzi wa Sera na Utafiti wa Chama hicho, Chacha Mwita, alisema wajumbe waliokuwa wamefika walikuwa hawana uwezo wa kuruhusu kufanyika kwa mkutano huo. Mwita alisema idadi ambayo inatakiwa ya wajumbe wote ni zaidi ya 120, lakini waliokuwa wamefika walikuwa hawazidi 50.Popular Posts
-
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila amekanusha vikali madai kwamba alishinda uchaguzi wa nchi hiyo kupitia wizi wa kura...
-
Huduma ya Maji na Nishati (EWURA), Mhandisi Godwin Samwel, akizungumza na wanahabari jana jijini, Dar es Salaam kuhusu kupanda kwa bei za m...
-
Pope Benedict XVI is in the Spanish capital, Madrid, for four days of events expected to be attended by hundreds of thousands of people. ...
-
Mkesha ulofanyika katika uwanja wa Taifa wa mpira katika kuliombea Taifa
-
Waziri wa Usalama wa Nchi, George Saitoti, alisema jeshi litawasaka wafuasi wa kikundi cha waislamu wenye siasa kali, al Shabaab, kokote wa...
-
Maandamano kupinga uroho wa makampuni yamefanywa sehemu mbali mbali za dunia, yakitiwa moyo na maandamano ya wiki mbili sasa yanayofanywa N...
-
Katika kuitikia kaulimbiu ya kilimo kwanza Kampuni ya Utalii ya Cordial Tours Yenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam imeamua kuunga Mk...
-
ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ambaye anatumikia kifungo cha miaka miwili je...
-
MWANASIASA machachari ambaye pia ni Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Mu...
-
Mwanamfalme wa Uingereza Charles na mkewe Camilla, au The Prince of Wales and The Duchess of Cornwall, kama wanavyojulikana rasmi, watafany...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)




0 comments:
Post a Comment