SERIKALI imeamua kuunda kikosikazi kitakachohusisha Idara ya Usalama wa Taifa, Polisi wa Kimataifa (Interpol) na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kwa ajili ya kuanza uchunguzi kuhusu Watanzania wanaotuhumiwa kuficha kiasi cha Sh314 bilioni nchini Uswisi. Hatua hiyo ya uchunguzi inatokana na Bunge kutoa maazimio ya kuitaka Serikali kufuatilia sakata hilo katika kikao chake kilichopita mjini Dodoma na kutoa majibu katika kikao cha Bunge cha Aprili mwakani. Akizungumza na Mwananchi Jumapili jana, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Jaji Frederick Werema alisema, “Tuhuma hizo siyo jambo dogo na Serikali haiwezi kuzipuuza, sasa tunachukua hatua madhubuti.” Jaji Werema alisema kuwa Serikali imeshapiga hatua katika kufanya uchunguzi huo. “Tumepiga hatua katika suala hili, ila ukianza kusema sana utakuwa unaharibu. Tumeamua kuwa na kikosi maalumu cha upelelezi kitakachoshirikisha Idara ya Usalama wa Taifa, Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) na Wizara ya Fedha na wachunguzi binafsi wakiwamo Polisi wa Kimataifa (Interpol) pamoja na Benki ya Dunia (WB). “Serikali inaweza kuwashirikisha watu wengine kama Benki ya Dunia (WB) na Polisi wa Kimataifa (Interpol) kwa ajili ya kusaidia uchunguzi huo.” Aliongeza kuwa katika timu hiyo, wameamua kumshirikisha Mbunge wa Kigoma Kaskazini, Zitto Kabwe ambaye amekuwa mstari wa mbele katika kutaka ukweli wa sakata hilo. “Tumeamua kulifuatilia jambo hili, kama tutafanikiwa litakuwa jambo jema. Kama hatutafanikiwa tutakuwa tumejaribu,” alisema. Hata hivyo, Werema alisema kuwa, bado hawajamwita Zitto ambaye pia ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema kwa ajili ya ushauriano zaidi. “Unajua kuwa mwanasheria mkuu siyo kujua kila kitu, Zitto pia anaweza akawa na mbinu, ambazo zitasaidia katika jambo hili,” alisema Werema.
Popular Posts
-
What to do in Zanzibar when you’re a tourist? I had booked myself a 4-day trip to the island, and, taking the advice of friends and a quic...
-
MKUTANO MKUU TASWA DESEMBA 21 NA 22 Kiromo, BAGAMOYO
-
Takribani watu 24 wamekufa baada baada ya maporomoko yanayotokana na mvua za masika kutokea mashariki mwa Ugadna, wafanyakazi wa Shirika la...
-
Sheikh Mkuu wa Bakwata, Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kushoto), akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki katika Ma...
-
Newcastle imetoka sare ya 0-0 na Arsenal katika mchezo uliokuwa na kasoro za hapa na pale. Katika mchezo huo mshambuliaji wa Arsenal kuto...
-
The company behind Blackberry phones, Research In Motion (RIM) unveiled two new Blackberry Bold smartphones today as well as a new Blackber...
-
RAIS Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wakuu kutoka cheo cha Meja Jenerali kuwa Luteni Jenerali kuanzia Novemba 21,mwaka huu. K...
-
MTUNZI na mwigizaji wa filamu za Swahiliwood, Omary Clayton 'Ommy' ,amesisitiza kuwa yeye ndiye mwandishi wa filamu ya Shakira il...
-
On Monday, fans got their first look at Jay-Z and Kanye West’s new collaboration album, “Watch the Throne.” However, another Kanye controv...
-
KUTOKANA na kile kichoonekana ni kutaka kukabiliana na uhaba wa sukari na kupanda kwa bei yake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajia kukuta...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)
0 comments:
Post a Comment