WIZARA ya Nishati na Madini, imesema tatizo la umeme nchini linatokana na kuchoka kwa miundombinu na hivyo kuzidiwa nguvu. Kauli hiyo imekuja siku kadhaa baada ya baadhi ya vyombo vya habari, kutangaza kuwepo kwa mgao wa umeme nchini. Akizungumza jijini Dar es Salaam jana, Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Eliakim Maswi, alisema mgao ulijitokeza za katika Mkoa wa Dar es Salaam, ulisababishwa na kuungua kwa transfoma mbili zenye ukubwa wa 15 MVA na Kv 33/11 zilizopo katikati ya Jiji. Alisema tatizo hilo lilianza Machi 6 mwaka huu ambapo umeme ulikatika kutokana na hitilafu katika kituo cha kupoozea umeme ilichoko mkabala na Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu. Maswi alisema baada ya hitilafu hiyo, Serikali iliamua kugharamia manunuzi ya ya transfoma nne zenye thamani ya Dola 350 milioni kwa utaratibu wa dharura. Kuhusu deni la Tanesco la Sh 279 bilioni, alisema deni hilo si la kweli na kwamba deni halisi ni Sh 79 bilion. “Deni tunalodaiwa ni Sh 79 bilioni lakini wao wamejulisha hadi madeni ya miradi ambayo imeingia mikataba na shirika pamoja na makampuni ambazo zinafanya kazi na shirika letu,”alisema na kuongeza Katika hatua nyingine, wizara ipo katika mkakati wa kuongeza megawati 100 za umeme ili kufikia megawati 1370 Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Tanesco, William Mhando, alisema baada ya kupata Sh 408 bilioni shirika linajipanga kubadilisha miundombinu yake.
Popular Posts
-
What to do in Zanzibar when you’re a tourist? I had booked myself a 4-day trip to the island, and, taking the advice of friends and a quic...
-
MKUTANO MKUU TASWA DESEMBA 21 NA 22 Kiromo, BAGAMOYO
-
Takribani watu 24 wamekufa baada baada ya maporomoko yanayotokana na mvua za masika kutokea mashariki mwa Ugadna, wafanyakazi wa Shirika la...
-
Sheikh Mkuu wa Bakwata, Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kushoto), akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki katika Ma...
-
Newcastle imetoka sare ya 0-0 na Arsenal katika mchezo uliokuwa na kasoro za hapa na pale. Katika mchezo huo mshambuliaji wa Arsenal kuto...
-
The company behind Blackberry phones, Research In Motion (RIM) unveiled two new Blackberry Bold smartphones today as well as a new Blackber...
-
RAIS Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wakuu kutoka cheo cha Meja Jenerali kuwa Luteni Jenerali kuanzia Novemba 21,mwaka huu. K...
-
MTUNZI na mwigizaji wa filamu za Swahiliwood, Omary Clayton 'Ommy' ,amesisitiza kuwa yeye ndiye mwandishi wa filamu ya Shakira il...
-
On Monday, fans got their first look at Jay-Z and Kanye West’s new collaboration album, “Watch the Throne.” However, another Kanye controv...
-
KUTOKANA na kile kichoonekana ni kutaka kukabiliana na uhaba wa sukari na kupanda kwa bei yake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajia kukuta...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)
0 comments:
Post a Comment