NEEMA imeendelea kumdondokea mwanamuziki Chaz Baba ambaye baada ya kuhamia Bendi ya Mashujaa Musica na kuvuta mkwanja mrefu, sasa amechaguliwa kuwa rais wa bendi hiyo. Kuchaguliwa kuwa rais wa bendi, maana yake ni kuwa mfuko utazidi kutuna kwa kuwa cheo hicho ni lazima kiendane sambamba na marupurupu. Akizungumza na gazeti hili Mkurugenzi wa bendi hiyo, Max Luhanga amesema, kwa kuwa majukumu ya Chaz Baba yameongezeka ni wazi kuwa marupurupu yataongezeka ingawa mpaka sasa bado hawajaamua ni kwa kiasi gani watamuongezea mshiko. "Hivi sasa Chaz atakuwa na kazi nyingi, lakini hadhi ya cheo ni lazima iendane na mapato, huwezi kumwita rais halafu akawa choka mbaya, lengo letu ni kuboresha maisha ya wanamuziki wetu pia," anasema Max. Chaz Baba aliibuka kidedea kwa kura 19 dhidi ya 26 zilizopigwa na kuwabwaga wanamuziki wenzake Sauti ya Radi na Mirinda Nyeusi. Rais Chaz Baba anachukua nafasi hiyo iliyokuwa inashikiliwa na mwanamuziki mwenzake anayefahamika kwa jina moja la Kajo. Hata hivyo kuingia madarakani kwa Chaz Baba pia kumemsababishia rais wa zamani, Kajo kutimuliwa kwa kundini kwa kile ambacho mkurugenzi anasema ni utovu wa nidhamu. Max anasema baada ya Chaz Baba kuchaguliwa, Kajo aligoma kutoa ushirikiano kwa rais mpya ikiwemo kumkabidhi ofisi. Mbali na kuwa katika safu ya mbele ya uimbaji, Chaz Baba sasa anakuwa na majukumu ya kupanga programu za shoo, kupanga mavazi ya wanamuziki, kusikiliza na kusimamia maoni, ushauri na kutatua matatizo ya wanamuziki. Bendi hiyo inaongozwa na Mkurugenzi, Max Luhanga, Meneja, King Dodoo na Rais ni Chaz Baba kuanzia Machi 27.
Popular Posts
-
I: UTANGULIZI a) Masuala ya Jumla Mheshimiwa Spika, 1. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi M...
-
Mtaalamu kutoka Finland asaidia mikakati ya tehama
-
WIZARA ya Nishati na Madini, imesema tatizo la umeme nchini linatokana na kuchoka kwa miundombinu na hivyo kuzidiwa nguvu. Kauli hiyo ...
-
Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma ya Bunge ya Hesbu za Mashirika ya Umma, Kabwe Zuberi Zitto, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma ...
-
NEW YORK, Marekani VIDEO iliyoonyweshwa mwishoni mwa wiki katika mitandao mbalimbali ya kijamii, ambayo ilielezea madhara ya taratibu ana...
-
JOSEPH KABILA Ni kijana na anawakilisha mustakabali wa nchi," Ndivyo walivyosema wafuasi wa Joseph Kabila wakati akiwasilisha fomu ...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)
0 comments:
Post a Comment