MFUMUKO wa bei unaweza kuwakimbiza wawekezaji wanaotaka kuja nchini kuwekeza rasilimali zao kama utaendelea kukua kama ilivyo sasa.Kwa sasa kiwango cha mfumuko wa bei, kimefikia asilimia 19. Tahadhari hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Benki ya Standard Chartered, Jeremy Awori, alipokuwa akiwasilisha mada yake katika semina ya Mameneja wa Rasilimali Watu kutoka kampuni mbalimbali. Semina hiyo iliyokuwa na lengo la kuangalia masuala mbalimbali ya rasilimali watu iliandaliwa na Chama cha Wanataaluma ya Rasilimali Watu Tanzania. Awori alisema tafiti zinaonyesha kuwa Tanzania ndiyo yenye mfumuko mkubwa wa bei miongoni mwa nchi za Afrika Mashariki, jambo linaloweza kuathiri biasharana za uwekezaji.“Mfumuko wa bei ukiwa juu mwekezaji analinganisha na nchi nyingine akiona kule hakuna mfumuko mkubwa anajiuliza kwanini niwekeze hapa ambapo itanigharimu sana wakati kuna nchi mfumuko uko chini na anaweza kufanyabiashara vizuri, maana mfumuko wa bei unasababisha gharama kubwa hata unapoajiri watu,” alisema. Pia alisema Tanzania ina fursa ya kukuza uchumi wake kwa kiwango kikubwa hasa ikizingatiwa kuwa imejaliwa kuwa na rasilimali nyingi kuliko nchi nyingi za Afrika.Alisema Tanzania ina madini mengi na maliasili nyingi ambazo hazipatikani katika nchi nyingi na kwamba hiyo ni fursa kubwa ya kuwezesha uchumi kupaa kwa haraka. “Kuna vitu vingine huhitaji kuambiwa, hivi nani asiyejua kuwa Tanzania imejaa madini na maliasili za kutosha, tukivitumia hivi vizuri inaweza kuwa njia ya kutosha kuondokana na hali iliyopo sasa,” alisisitiza.Awori alisema biashara kati ya Tanzania na mataifa makubwa kama China, inaongezeka na kwamba kuna haja kwa wanataaluma kuichukua hiyo kama fursa kwao. Alitoa mfano kuwa Wachina wengi wanakuja Tanzania kuendesha miradi mikubwa katika sekta mbalimbali kama ujenzi na kwamba wanahitaji huduma mbalimbali kama za kibenki.
Popular Posts
-
Mkesha ulofanyika katika uwanja wa Taifa wa mpira katika kuliombea Taifa
-
President Robert Mugabe scoffed Saturday at calls for him to retire, saying he will remain in power until his Zanu PF party wins elections...
-
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila amekanusha vikali madai kwamba alishinda uchaguzi wa nchi hiyo kupitia wizi wa kura...
-
Huduma ya Maji na Nishati (EWURA), Mhandisi Godwin Samwel, akizungumza na wanahabari jana jijini, Dar es Salaam kuhusu kupanda kwa bei za m...
-
Pope Benedict XVI is in the Spanish capital, Madrid, for four days of events expected to be attended by hundreds of thousands of people. ...
-
Dar es Salaam. Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka amesema mwezi ujao wanatarajia kutangaza kima cha chini cha mshahara kwa wafany...
-
Waziri wa Usalama wa Nchi, George Saitoti, alisema jeshi litawasaka wafuasi wa kikundi cha waislamu wenye siasa kali, al Shabaab, kokote wa...
-
Maandamano kupinga uroho wa makampuni yamefanywa sehemu mbali mbali za dunia, yakitiwa moyo na maandamano ya wiki mbili sasa yanayofanywa N...
-
Katika kuitikia kaulimbiu ya kilimo kwanza Kampuni ya Utalii ya Cordial Tours Yenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam imeamua kuunga Mk...
-
MWANASIASA machachari ambaye pia ni Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Mu...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)




0 comments:
Post a Comment