BAADHI ya wananchi wa Ubungo katika Manispaa ya Kinondoni, jana wavamia Ofisi za Kampuni inayosambaza maji katika Jiji la Dar es Salaam na baadhi ya maeneo ya Mkoa wa Pwani (Dawasco), kulalamikia kukosa huduma za maji. Katika tukio hilo, wananchi hao waliongozwa na mbunge wao John Mnyika na kwa mujibu wa maelezo yao, hatua hiyo ilikuja baada ya kampuni hiyo kutowapa majibu kuhusu malalamiko ya kukosa huduma .
Walisema miezi nane iliyopita, waliiandika kampuni hiyo kutaka kujuia sababu za wao kukosa huduma za maji katika maeneo yao, lakini hawakujibiwa. Mmoja wa wananchi hao Msafiri Shabani wa Mabibo, alielezea kushangazwa kwake na hatua ya wananchi katika eneo hilo kukosa maji wakati huko nyuma walikuwa wanapata huduma.
“Huko nyuma tulikuwa tunapa huduma angalau wiki mara tatu lakini kwa sasa tunapata mara moja na yanafunguliwa kwa saa mbili tu, nadhani kuna mchezo fulani unafanyika, ili tukosema maji,” alisema. Akijibu tuhuma hizo Mkurugenzi Mtendaji wa Dawasco, Mhandisi Jackson Midala alikiri ofisi yake kupokea malalamiko ya wananchi hao kuhusu kukosa huduma ya maji, lakini alisema hiyo inatokana na upungufu wa maji yanayohitajika.
Alisema si kweli kwamba Dawasco inashirikiana na watu wanaodaiwa kuuza maji na hivyo wakati mwingine kukuta wakiwafungia watu mabomba ili wafanye biashara.
Kuhusu suala la mabomba maarufu ya kichina ambao ni mradi uliotekelezwa na Wachina, alisema ni kweli baadhi ya sehemu hayatoi maji, lakini wanakwenda hatu kwa hatua ili hatimaye waweze kutoa huduma za ukakika.. Hata hivyo alisema hawezi kuzungumzia tuhuma zilizotolewa na wananchi hao dhidi ya meneja wa Dawasco Boko, lakini akasema kwamba inabidi azifanyie kazi .
Kuhusu mgawo wa maji alisema hauepukiki kwani wakati mwingine wanaamua kufanya mgawo wa maji mfano Manzese siku tatu ili wengine pia wapate mwisho
0 comments:
Post a Comment