WAKATI mpango wa mwaka mmoja wa umeme wa dharura ukiwa umemalizika, utekelezaji wake umeshindwa kufikiwa na matokeo yake tatizo la mgawo umeme usiotabirika linaendelea nchini. Serikali na Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) wameshindwa kutoa majibu sahihi kuhusiana na kukwama kwa mradi huo. Alipoulizwa kuhusu maendeleo ya mpango huo, Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi alisema, “Leo ni Jumamosi, nipo kanisani. Naomba uniache kwanza, tena nisingependa kuzungumzia suala hilo kabisa.” Gazeti hili lilimtafuta Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo kwa njia ya simu lakini hakupokea na badala yake alituma ujumbe mfupi wa maneno uliosomeka, “I am in meeting (nipo kwenye mkutano).” Naye Kaimu Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Tanesco, Felschami Mramba alisema kuwa haiwezekani kukawa na mpango wa dharura wa mwaka mmoja akieleza kuwa madhara humalizika tatizo husika linapokuwa limekwisha. “Huu mpango wa dharura utakwisha siku ambayo bomba la gesi kwa ajili ya kuzalisha umeme litakapofika Dar es Salaam likitokea Mtwara,” alisema. Waziri Muhongo Akiwasilisha bajeti ya wizara yake katika Bunge la Bajeti mwaka huu, Profesa Sospeter Muhongo alisema kuwa wizara yake imeendelea kuchukua hatua mbalimbali kuboresha upatikanaji wa nishati ya umeme nchini. Alisema hadi Juni 2012 uwezo wa mitambo ya kufua umeme ulikuwa megawati 1,375.74, gesi asili asilimia 40, maji ( 41) na mafuta (19). Alieleza kuwa uwezo huo ni ongezeko la megawati 367 sawa na asilimia 36 ikilinganishwa na uwezo wa megawati 1,013.74 uliokuwapo Juni, 2011. Mahitaji ya juu ya umeme kwa mwaka 2011/12 yalifikia wastani wa megawati 820.35, ikilinganishwa na megawati 730 kwa mwaka 2010/11. Uhaba huo wa umeme ndiyo ulizaa Mpango wa Dharura wa Kuondoa Mgawo wa Umeme nchini ulioridhiwa na Bunge. Katika Mpango huo, jumla ya megawati 572 zilipangwa kuzalishwa na kuingizwa kwenye Gridi ya Taifa. Mitambo iliyotumika kuzalishia umeme huo ni Symbion megawati 137, Aggreko (100), IPTL (80) na ule wa Gesi Asili wa Ubungo (105).
Popular Posts
-
What to do in Zanzibar when you’re a tourist? I had booked myself a 4-day trip to the island, and, taking the advice of friends and a quic...
-
MKUTANO MKUU TASWA DESEMBA 21 NA 22 Kiromo, BAGAMOYO
-
Takribani watu 24 wamekufa baada baada ya maporomoko yanayotokana na mvua za masika kutokea mashariki mwa Ugadna, wafanyakazi wa Shirika la...
-
Sheikh Mkuu wa Bakwata, Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kushoto), akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki katika Ma...
-
Newcastle imetoka sare ya 0-0 na Arsenal katika mchezo uliokuwa na kasoro za hapa na pale. Katika mchezo huo mshambuliaji wa Arsenal kuto...
-
The company behind Blackberry phones, Research In Motion (RIM) unveiled two new Blackberry Bold smartphones today as well as a new Blackber...
-
RAIS Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wakuu kutoka cheo cha Meja Jenerali kuwa Luteni Jenerali kuanzia Novemba 21,mwaka huu. K...
-
MTUNZI na mwigizaji wa filamu za Swahiliwood, Omary Clayton 'Ommy' ,amesisitiza kuwa yeye ndiye mwandishi wa filamu ya Shakira il...
-
On Monday, fans got their first look at Jay-Z and Kanye West’s new collaboration album, “Watch the Throne.” However, another Kanye controv...
-
KUTOKANA na kile kichoonekana ni kutaka kukabiliana na uhaba wa sukari na kupanda kwa bei yake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajia kukuta...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)
0 comments:
Post a Comment