KAMBI ya Upinzani Bungeni, jana ilimlipua Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Mifugo, Dk E. J. Sekidio kwa kutoa vibali vya kuagiza tani 127 za nyama ya kuku kutoka nje ya nchi, hasa kutoka Brazil.
Kwa mujibu wa kambi hiyo, uagizaji huo wa kuku ni kinyume cha sheria za nchi na matamko mbalimbali yanayotolewa mara kwa mara bungeni na Serikali.
Suala hilo liliibuliwa bungeni jana na Msemaji wa kambi hiyo, Sylvester Kasulumbai, wakati akiwasilisha maoni ya kambi hiyo kuhusu bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi iliyowasilishwa na waziri wake, Dk David Mathayo David.
Kasulumbai alisema Aprili 5 mwaka huu mkurugenzi huyo alitoa kibali namba 000551 kwa kampuni ya Frostan Ltd ya jijini Dar es Salaam kuagiza tani 27.1 za nyama ya kuku kutoka Brazil.
Alisema Julai 20 mwaka huu, mkurugenzi huyo pia alitoa kibali kingine chenye namba 00000409 kwa Kampuni ya Malik Faraji, kuagiza tani 100 za nyama ya kuku kutoka Zanzibar.
Kwa mujibu wa msemaji huyo, tani hizo 100 za nyama za kuku zilizoagizwa kutoka Zanzibar zilikuwa ni kwa ajili ya migodi ya madini ya Barrick.
“Taarifa zinaonyesha kuwa Tanzania ina kuku takribani milioni 58 wanaofugwa, lakini pamoja na kuku wote hao bado wizara imeendelea kutoa vibali vya kuagiza kuku kutoka Brazil,”alisema.
Kambi hiyo iliitaka Serikali kutoa maelezo kama ni sahihi kuendelea kutoa vibali vya kuagiza kuku kutoka nje ya nchi wakati nchi ina wafugaji
wa kuku.
“Tunataka kujua nyama za kuku kiasi cha tani 100 zilizoagizwa kutoka Zanzibar ni kutoka nchi gani na kama ni kutoka Zanzibar, kwanini wanahitaji kibali kusafirisha nyama kuja bara,”alisema.
Kambi hiyo pia imekilipua kiwanda cha sukari cha Kagera Sugar kwa kutumia ekari 45,000 ilizopewa na Serikali. kulikodisha kwa wafugaji wa Rwanda na Uganda.
Kasulumbai alifafanua kuwa vitalu vya Ranchi ya Kitengule viligawiwa kwa wafugaji wawekezaji wadogo wadogo ambapo kila mmoja alipata kati ya hekta 2,000 na 3,000.
“Lakini cha ajabu kiwanda cha Kagera Sugar kilipewa hekta 45,000 wakati kiwanda hicho hakina mifugo kwa kisingizio tu cha kutaka kulima miwa ndani ya eneo hilo la ufugaji,” alisema.
Kasulumbai alisema kiwanda hicho hivi sasa kinatumia eneo hilo kukodisha wafugaji wa Rwanda na Uganda, ilihali wafugaji wa Tanzania wakikosa eneo la kulishia mifugo yao.
Wapinzani wamlipua Mkurugenzi wa Mifugo
Jitokezedirectory
Friday, August 10, 2012
Popular Posts
-
JAJI Mkuu, Mohamed Chande Othman ameeleza sababu za kutokuwa kwenye jopo la majaji waliopangwa kusikiliza kesi ya aliyekuwa mbunge wa Cha...
-
Rais Dk.Kikwete akisimikwa rasmi kuwa chifu wa kabila la wabena katika sherehe za kuzindua mkoa mpya ...
-
NEEMA imeendelea kumdondokea mwanamuziki Chaz Baba ambaye baada ya kuhamia Bendi ya Mashujaa Musica na kuvuta mkwanja mrefu, sasa amechag...
-
Katika kuitikia kaulimbiu ya kilimo kwanza Kampuni ya Utalii ya Cordial Tours Yenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam imeamua kuunga Mk...
-
SERIKALI itatoa leseni kwa wafanyabiashara wa hapa nchini, ili kuwawezesha kuagiza tani 120,000 za sukari kutoka nje ya nchi na sukari hiyo...
-
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimjulia hali mtoto Andrew Simba(15) aliyelazwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili wakati Rais alipowate...
-
Rap icon Tupac Shakur covers the latest issue of XXL in a profile that celebrates the rapper, who passed away 15 years ago. In the latest...
-
MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), imezikutanisha kampuni za mafuta hapa nchini kwa lengo kuunda Bodi ya Wakurugenzi ya Kampu...
-
Uingereza imesitisha kwa muda msaada iliyokuwa iipe Rwanda kwa sababu ya wasiwasi kuhusu kuhusika kwa nchi hiyo katika mzozo uliopo Jam...
-
Mwanaharakati wa haki za binadamu nchini Kenya Al-Amin Kimathi ni miogoni mwa washukiwa watano wa shambulio la bomu la mjini Kampala wakati...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)
0 comments:
Post a Comment