Nyaraka za Libya zafichua siri

Sunday, September 4, 2011


Nyaraka zilizonekana katika jengo la serikali ya Libya mjini Tripoli, zinaonesha uhusiano wa karibu baina ya mashirika ya ujasusi ya mataifa ya magharibi na serikali ya Kanali Muammar al-Gaddafi.


Makabrasha hayo yaliyopatikana na shirika la kupigania haki za kibinaadamu lenye makao yake Marekani, Human Rights Watch, yanaonesha mawasiliano ya barua baina ya idara ya ujasusi ya Libya, na CIA, ya Marekani na MI6 ya Uingereza, pamoja na mashirika mengine.

Afisa wa Human Rights Watch aliyeona nyaraka hizo, aliishutumu CIA kuwa watu kadha iliyowakamata kwa tuhuma za ugaidi iliwapeleka Libya, na kwamba shirika hilo lilikuwako wakati watu hao wakihojiwa.

Nchini Uingereza, Waziri wa Mashauri ya Nchi za Nje, amejibu tuhuma kuwa majasusi wa Uingereza walimpa Kanali Gaddafi taarifa kuhusu wapinzani wake.

William Hague alisema tuhuma hizo zinahusu serikali ya zamani ya Uingereza.

0 comments:

Post a Comment