Ewura kunda bodi ya kuagiza mafuta pamoja

Friday, September 16, 2011


MAMLAKA ya Udhibiti wa Nishati na Maji (Ewura), imezikutanisha kampuni za mafuta hapa nchini kwa lengo kuunda Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni tanzu itakayounganisha wamiliki wa kampuni hizo, itakayokuwa na jukumu la kuugiza mafuta kwa pamoja.Lengo la muungano wa kampuni hizo ni kutaka kuondoa wingu kila kampuni ya mafuta, kuangiza mafuta peke yake.

Chini ya mpango huo, kampuni hizo sasa zitakuwa zikiangiza mafuta kwa utaratibu wa zabuni.
Akizungumza na wadau wa kampuni za mafuta jijini Dar es Salaam jana, Kamishna Msaidizi inayeshughulikia Petroli na Gesi, Prosper Victus alisema kuanzishwa kwa kampuni hiyo kutatoa fursa kwa kila kampuni, kuagiza mafuta kwa oda kupitia chombo hicho.

Alisema kampuni hiyo pia itasaidia serikali kupata uhakiki wa kubaini ni kiasi cha mafuta kinachotumika nchini.
Kwa mujibu wa Victus, kuanzishwa kwa kampuni hiyo pia kutasaidia kupunguza msongamano wa meli bandari na kubaini gharama za mafuta yanayoagizwa nchini.

"Lakini pia utasaidia nchi kukusanya kodi na kuongeza ufanisi wa uagiziaji wa mafuta kwa uratatibu wa malipo ya zabuni.Victus alisema kama mafuta yakiagiza kwa pamoja bei itakuwa nafuu kwa upande wa sehemu za uhifadhi kwa gharama ya dola 20,000 iliyokuwa ikitozwa kwa mwezi.

Alisema kuanzishwa kwa kampuni hiyo pia kutatoa nafasi ya kuongeza matuminzi ya bandari na kusaidia nchi nyingi jirani kuagiza mafuta kutoka Tanzania.

Hata hivyo Vitus alisema kuwa changamoto ya usafirshaji mafuta nchini ni kubwa kiuchumi kutokana na hali ya miundombinu iliyopo nchini na wamba kama zitafanyiwa kazi, itasaidia kuboresha hifadhi za mafuta.

Alisema Tanzania ina sehemu kubwa ya kuhifadhia mafuta kuliko Kenya ambayo ina hifadhi ya mafuta kama ya Zambia.Victus alisema utaratibu wa kuanzisha kampuni si mpya kwamba uliwahi kufanyika mwaka 1997 na ulileta mafanikio makubwa.

0 comments:

Post a Comment