SHIRIKA la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) halijapata hasara yoyote katika miradi yake tangu utawala wa awamu ya nne ulipoingia madarakani, Bunge lilielezwa jana.Naibu Waziri wa Kazi na Ajira, Dk Makongoro Mahanga alisema kuwa katika kipindi hicho, NSSF imepata faida ya uwekezaji kutoka Sh 424.899 bilioni kati ya mwaka 2005/06 na kufikia Sh1.029,206 bilioni kwa mwaka 2009/010.
Naibu Waziri alisema katika kipindi hicho pia Shirika hilo lilipa Sh 339.09 bilioni kwa ajili ya kulipia mafao mbalimbali kwa wanachama wake.Katika swali la msingi, David Kafulila (Kigoma Kusini-NCCR Mageuzi) alitaka kujua ni kwa kiasi gani watumishi ambao ni wanachama wa shirika hilo wanapata faida na hasara gani kutokana na uwekezaji wa NSSF.
Mbunge huyo pia alitaka kujua tangu Serikali ya awamu ya nne iingie madarakani ni hasara kiasi gani imepatikana katika shirika hilo
0 comments:
Post a Comment