Rais Dk.Kikwete akisimikwa rasmi kuwa chifu wa kabila la wabena katika sherehe za kuzindua mkoa mpya wa njombe pichani akipewa mkuki maalum kama ishara ya kuwa chifu kamili.
Rais DK. Kikwete akibonyeza kitufe huku wazeee wakirusha njiwa kuwa sasa njombe ni mkoa mpya wa kabila la wabena.
Chifu mpya wa kabila la wabena Rais jakaya kikwete akishuka jukwaani mara baada ya kuzindua mkoa. mpya wa njombe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwahutubia Vijana waliojiajiri kwa kazi ya kuendesha pikipiki za kupakia abiria maarufu kama Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam (hawapo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.Mh. Lowassa alikuwa ni Mgeni Rasmi katika hafla hiyo iliyofana sana.
Naibu Waziri wa Kazi na Ajira,Mh. Dkt. Makongoro Mahanga akizungumza machache kwenye Tamasha hilo kabla ya Kumkaribisha Mgeni Rasmi kwenye Tamasha hilo,Mh. Edward Lowassa (kulia).Katikati ni Kamanda wa Polisi Kitengo cha Usalama Barabarani Tanzania,DCP. Mohammed R. Mpinga.
Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki Wilaya ya Ilala,Michael Roewe akisoma Risala yao mbele ya Mgeni Rasmi,Mh. Edward Lowassa (hayupo pichani) wakati wa Tamasha Maalum la Bodaboda lililofanyika leo kwenye Viwanja vya Leaders Club,jijini Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea Risala ya Chama cha Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam,Kutoka kwa Mwenyekiti wa Chama cha Waendesha Pikipiki Wilaya ya Ilala,Michael Roewe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi Zawadi kwa Afisa wa Benki ya FNB kwa kutoa Mchambo mkubwa kwa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akikabidhi Zawadi kwa Afisa wa Mfuko wa PSPF kwa kutoa Mchambo mkubwa kwa Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akipokea Zawadi Kutoka kwa Mwenyekiti wa Muda wa Shirikisho la Waendesha Bodaboda Mkoa wa Dar es Salaam,Said Magamba.
Salamu kwa waendesha Bodaboda.
Wasanii wa Muziki wa Kizazi Kipya wanaounda kundi la KIBEGA,wakitoa Burudani mbele ya Waendesha Bodaboda hao.
Sehemu ya Waendesha Bodaboda hao wakifatilia kwa makini hotuba ya Mgeni Rasmi.
Msanii Linex akifanya yake Viwanjani hapo mapema leo.
Mgeni Rasmi katika Tamasha la Waendesha Bodaboda Mkowa wa Dar es Salaam,Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiondoka viwanjani hapo huku Vijana Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam wakimsindikiza kwa shangwe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akiwaaga Vijana wa Bodaboda wa Mkoa wa Dar es Salaam wakati alipokuwa akiondoka viwanjani hapo huku shangwe zikitawala viwanjani hapo.
Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotion inayoandaa tamasha la Krismas Bw. Alex Msama akitoa ufafanuzi kwa waandishi wa habari kuhusu tamasha hilo.
Rais wa Zanzibar na wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akisalimiana na Mwenyekiti wa UVCCM Taifa Sadifa Juma Khamis,alipowasili katika uwanja wa Mpira Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba,katika ufunguzi wa matembezi Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar katika kuadhimisha miaka 5o ya Mapinduzi.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,akisalimiana na Naibu Katibu Mkuu wa UVCCM Zanzibar Shaka Hamdu Shaka,alipowasili katika uwanja wa Mpira Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba,katika ufunguzi wa matembezi Umoja wa Vijana wa CCM Zanzibar katika kuadhimisha miaka 5o ya Mapinduzi.[Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
Vijana wa UVCCM wakiwa wamebeba Pich za Viongozi wa Chama katika Matembezi ya Madhimisho ya miaka 5o ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, yaliyofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,na Makamo Mwenyekiti wa CCM Zanzibar,(hayupo pichani)kuanzia Micheweni kuelekea Wete Mkoa wa Kasakazini Pemba. [Picha na Ramadhan Othman Ikulu.]
Mechi ya Nani Mtani Jembe kati ya Yanga na Simba iliyochezwa juzi (Desemba 21 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam na Simba kuibuka na ushindi wa mabao 3-1 imeingiza sh. 422,611,000.
Mapato hayo ni kutokana na washabiki 52,589 waliokata tiketi kushuhudia mechi hiyo kwa viingilio vya sh. 5,000, sh. 7,000, sh. 10,000, sh. 15,000, sh. 20,000 na sh. 40,000. Kiingilio cha sh. 5,000 ndicho kilichovutia watazamaji wengi ambapo walikuwa 19,044.
Asilimia 18 ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) iliyolipwa kutokana na mapato hayo ni sh. 64,466,084.75 wakati gharama za kuchapa tiketi ni sh. 7,488,000.
Mgawo mwingine ilikuwa kama ifuatavyo; kila klabu imepata sh. 117,470,066.61, asilimia 15 ya uwanja ni sh. 52,598,537.29, Mfuko wa Maendeleo ya Mpira wa Miguu (FDF) sh. 35,065,691.53 wakati gharama za mchezo zilikuwa sh. 28,052,553.22.
MALINZI, MKUTANO WA WAANDISHI WA HABARI
Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Jamal Malinzi atakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho (Desemba 24 mwaka huu).
Mkutano huo utafanyika saa 6 kamili mchana kwenye ukumbi wa mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).
Boniface Wambura Mgoyo
Kaimu Katibu Mkuu
Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF)
Juma Kaseja `Tanzania One` amekingiwa kifua na bosi wake ,Yussuf Manji baada ya kufungwa mabao matatu jana kwenye mechi ya Nani Mtani Jembe
na Salesi Malula
MWENYEKITI wa klabu ya Yanga, Yussuf Manji amemkingia kifua mlinda mlango wao mpya, Juma Kaseja baada ya kufungwa mabao matatu jana akiwa langoni katika mchezo wa Nani Mtani Jembe dhidi ya watani zao wa jadi, Simba Sc ambao Mnayama alishinda 3-1.
Mbao ya Simba sc katika mechi ya jana yalifungwa na Amis Tambwe aliyepiga mawili na kiungo Juma Awadh Issa, wakati la Yanga lilifungwa na Emmanuel Okwi.
Akizungumza leo na waandishi wa habari, Manji amasema hawakumsajili Kaseja kwa ajili ya kuifunga Simba SC, bali malengo yao ni kupata msaada wake katika michuano mikubwa ya soka barani Afrika.
Baada ya Yanga kufungwa jana, huku Kaseja akiwa langoni, katibu mkuu wa baraza la wazee la klabu hiyo, Mzee Ibrahim Akilimali, iliulaumu uongozi kwa kusema kuwa usajili wa kipa huyo ni makosa na hauna baraka zao.
Manji amejibu mapigo na kueleza kuwa umri unazidi kumtupa mkono mzee Akilimali kwani ameshindwa kukumbuka kuwa , huyo Ivo mwenyewe aliondoka Yanga akiwa anatumikia adhabu ya kufungiwa miezi sita na uongozi wa wakati huo kwa tuhuma za kufungisha kwenye mechi dhidi ya Simba SC.
Pia Manji alihoji wakati Simba ikisawazisha mabao yote matatu katika mchezo wao wa ligi kuu soka Tanzania bara oktoba 20 dhidi ya Simba sc , Kaseja alikuwa langoni?.
Mwenyekiti huyo alisema si jambo zuri kulaumiana pale yanapotokea makosa, bali ni kuwa na mshikamano kwa ajili ya maendeleo ya Yanga.
“Tunaheshimu uwezo wa Kaseja, thamani yake ni kubwa. Hakuna kipa yeyote nchini aliyedaka mechi nyingi za kimataifa kama kipa huyu. Kamwe hatuwezi kumshusha thamini yake na uwezo wake kwa kufungwa mabao matatu kwenye mechi ya jana ambayo ilikuwa sawa na bonanza tu”. Alisema Manji.
Manji alisema mechi ya jana walicheza kumfurahisha mdhamini wao, TBL, lakini haikuwa na maana yoyote na matokeo ya kufungwa wala hayajawaingia akilini.
Hata hivyo Manji amewapongeza Simba SC kwa kucheza soka safi, hivyo walistahili ushindi katika mchezo wa jana.
Kuelekea ngwe ya lala salama ya ligi kuu na michuano ya Kimataifa , Manji alisema wataboresha timu pamoja na benchi la ufundi kwa tafsiri ya kuwaondoa makocha wao Ernie Brandts na wasaidizi wake, Mzawa Fredy Felix Minziro na Mkenya, Mkenya Razack Ssiwa
“Timu itaenda tena Ulaya kuweka kambini kama walivyofanya waka jana. Naamini tutajivua vizuri na kuwa makali zaidi kutetea ubingwa wetu na kufanya vizuri michuano ya kimataifa”. Alisema Manji.
Ili kuongeza makali, Yanga imesajili wachezaji watatu katika dirisha dogo la usajili ambao ni mlinda mlango, Juma Kaseja, kiungo Hassan Dilunga na mshambuliaji mahiri raia wa Uganda, Emmanuel Anord Okwi.
Wachezaji hao walitumika jana, lakini hawakufua dafu mbele ya kikosi cha Simba Sc kilichoonekana kuwa bora zaidi Yanga.
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Mabibo, wilaya ya Kinondoni, Zakaria Kimemeneki (kulia), akikabidhi zawadi ya picha ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kwa Katibu wa Jumuia ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage, wakati wa kufungwa semina ya Baraza la UVCCM kata hiyo, jana. Picha hiyo imetolewa na UVCCM Mambibo, ili akabidhiwe Nape kutokana na kutambua mchango wake katika kuijenga CCM. Zaidi ya Vijana Wajumbe 30 walishiriki semina hiyo.
Kisha Mwenyekiti huyo akakabidhi picha ya Kamanda wa UVCCM Kata ya Mabibo, Dk. Fenella Mkandara ili nayo imfikie kwa kushukuru mchango wake kwa uilea jumuia hiyo ya Chama usiku na
mchana
Kisha Mwenyekiti huyo wa UVCCM akamvalisha Cholage kofia maalum ambayo UVCCM hao wanasema, walimuona kwa mara ya Kwanza katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana ameivaa ya aina hiyo baada ya kuteuliwa kushika wadhifa huo mjini Dodoma
Cholage akitoa kitabu cha Kanuni za UVCCM kwa mmoja wa washiriki wa semina hiyo. Kushoto ni Mwenyekiti wa CCM Kata ya Mabibo, Bononi Mlowe.
Wanasemina wakimsikiliza mgeni rasmi
Mgeni rasmi akivishwa skafu Cjolage, baada ya kuwasili kwenye ukumbi. Alisema hii ilikuwa mara yake ya kwanza kuvishwa skafu!!
MWENYEKITI wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Kata ya Mabibo, wilaya ya Kinondoni, Zakaria Kimemeneki (kulia), akikabidhi zawadi ya picha ya Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye, kwa Katibu wa Jumuiya ya Wazazi mkoa wa Dar es Salaam, Mohamed Cholage, wakati wa kufungwa semina ya Baraza la UVCCM kata hiyo, jana. Picha hiyo imetolewa na UVCCM Mabibo, ili akabidhiwe Nape kutokana na kutambua mchango wake katika kuijenga CCM. Zaidi ya Vijana Wajumbe 30 walishiriki semina hiyo. (Picha na Bashir Nkoromo).
NA BASHIR NKOROMO
UMOJA wa Vijana wa CCM, Kata ya Mabibo, Kinondoni jijini Dar es Salaam, umempongeza Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kwa kuwavua uongozi mawaziri wanne mwishoni mwa wiki.
UMOJA wa Vijana wa CCM, Kata ya Mabibo, Kinondoni jijini Dar es Salaam, umempongeza Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kwa kuwavua uongozi mawaziri wanne mwishoni mwa wiki.
Mawaziri waliovuliwa uongozi kufuatia Rais Kikwete kutengua teuzi wao ni, Dk. Emmanuel Nchimbi (Waziri wa Mambo ya Ndani), Shamsi Vuai (Waziri wa Ulinzi), Mathayo David Mathayo ( Mifugo na Maendeleo ya Uvuvi) na Khams Kagasheki (Maliasili na Utalii) ambaye ndiye pekee pamoja na uteuzi wake kutenguliwa na Rais lakini alitangaza kujiuzulu akiwa Bungeni.
Kutenguliwa kwa uteuzi wa mawaziri hao kulitangazwa rasmi Bungeni na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, hatua iyotokana na mapendekezo ya bunge, baada ya Kamati yake ya kudumu ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kubaini ‘uozo’ katika operesheni iliyofanyika hivi karibuni ya tokomeza ujangili.
Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)Dk. Willbroad Slaa jana December 22 alikua akihitimisha ziara yake ya kukagua uhai wa chama Igunga Mjini mkoani Tabora,mkutano huu uliofanyika katika uwanja wa Barafu.
Dk Emmanuel Nchimbi
chanzo gazeti la, Mwananchi
Kwa ufupi
- Kauli hiyo, imekuja baada ya ripoti iliyosomwa bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli ambayo imesababisha Rais Jakaya Kikwete kusitisha uteuzi wa mawaziri wanne.
Dar es Salaam. Jeshi la Polisi, limekiri kutikiswa na ripoti ya Operesheni Tokomeza Ujangili ambayo imemkumba Waziri wake wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Dk Emmanuel Nchimbi.
Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, Isaya Mungulu alisema jana kwamba operesheni hiyo imelitikisa jeshi hilo kutokana na madhara yaliyojitokeza wakati wa utekelezaji wake.
“Lengo la operesheni hiyo halikuwa kuleta madhara kwa wananchi, yaliyotokea ni changamoto kwa Polisi na sasa ni kujipanga upya ili haya yasije kutokea tena,” alisema na aliongeza: “Kwa sasa tunaziachia mamlaka husika ziendelee kulishughulikia suala hili kwa sababu limehusisha idara mbalimbali za Serikali.”
Kauli hiyo, imekuja baada ya ripoti iliyosomwa bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli ambayo imesababisha Rais Jakaya Kikwete kusitisha uteuzi wa mawaziri wanne.
Kauli hiyo, imekuja baada ya ripoti iliyosomwa bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli ambayo imesababisha Rais Jakaya Kikwete kusitisha uteuzi wa mawaziri wanne.
Mapema Novemba, mwaka huu, Spika wa Bunge, Anne Makinda aliunda Kamati ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira kuchunguza utekelezaji wa Operesheni Tokomeza Ujangili baada ya kutokea mjadala mkali bungeni kuhusu kadhia waliyopata wananchi.
Katika mjadala huo, wabunge walilalamikia watekelezaji wake wakisema ilitawaliwa na mateso kwani waliokuwa wakiiendesha walikuwa wakiwatesa wananchi na hata kusababisha vifo na majeruhi.
Taasisi zilizokuwa zikiendesha operesheni hiyo kabla ya kusitishwa ni; Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Polisi.
Kuzinduliwa kwa operesheni hiyo kulikuwa na lengo la kulinda rasilimali za nchi hasa tembo ambao katika siku za hivi karibuni wamekuwa wakiuawa kwa kasi na majangili kwa ajili ya pembe za ndovu.
Mwili wa binti aliyejinyonga, Zayana Mwamini(16), ukining'inia juu ya mti |
Kwa tarifa ambazo zimeifikia mtandao huu kutoka kwa dada wa binti huyo, Shamu Burohani, alisema kuwa, Zayana, alikutwa asubuhi Desemba 18 Mwaka huu akiwa amejinyonga na kamba za manila juu ya mti huo na mwili wake ulichukuliwa na Askari Polisi wa Kizuiani(maturubai) kwa uchunguzi zaidi.
Askari polisi wakiokoa mwili wa Zayana Mwamini aliyejinyonga kwa kamba ya manila hivi karibuni |
.“Baada ya kuondoka tulipoona harudi tulichukua hatua ya kumtafuta, bila mafanikio, ndipo ilipofika asubuhi ya Desemba 18, mwaka huu, majirani walituambia kuwa wamemuona juu ya mti ulioko na jirani na gesti ya Rondo, akiwa amejinyonga na kamba ya manila,” alisema Sham.
Shamu alisema kuwa ameishi na mdogo wake kwa miezi miwili sasa na kuwa alikuwa najifunza ufundi wa kushona nguo, lakini alianza tabia ya kutoka na kulala nje bila sababu yoyote .
Mwili wa binti huyo ulichukuliwa na Askari Polisi wa kituo cha Mbagala Kizuiani(maturubai) kwa uchunguzi zaidi.
Askari polisi wakiokoa mwili wa Zayana Mwamini aliyejinyonga kwa kamba ya manila hivi karibuni
Baadhi ya Mashuhuda wakiangalia mwili wa Zayana, aliyejinyonga kwa kamba. |
Askari Polisi wakipakia Mwili wa Zayana katika gari. |
Askari Polisi wakishusha mwili wa Zayana kutoka katika mti(Picha zote na Mathias Charles)
0 comments:
Post a Comment