WAZANZIBAR WAASWA KUTUNZA NA KUKUZA UTALII WA NDANI

Tuesday, December 4, 2012

Wananchi wameshauriwa kutekeleza agizo la Utalii kwa wote kwa kuyatembelea maeneo mbali mbali ya utalii Zanzibar ili kufahamu historia ya nchi ya Zanzibar kabla na baada ya Mapinduzi. Ushauri huo umetolewa na Mkuu wa Divisheni ya Makumbusho Zanzibar Khamis Abdallah Ali wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari katika ziara iliyojumuisha wanahabari na maafisa wa Makumbusho Amesema katika kutekeleza agizo la Utalii kwa wote wananchi wanapaswa kushajihishwa kutembelea maeneo ya kihistoria badala ya kuwaachia watalii peke yao kufanya ziara katika maeneo hayo. Amesema ni jambo la kusikitisha kuona wenyeji hawana hamu ya kujua historia ya nchi yao na kuwafanya wageni kujua historia ya Zanzibar kuliko Ameongeza kuwa Idara ya Makumbusho imeweka kiwango kidogo cha Shilingi 1000 ili kumrahisishia mwenyeji pale anapohitaji kwenda kutembelea maeneo ya makumbusho kwa ajili ya kujua historia ya nchi yao

0 comments:

Post a Comment