JAKAYA KUFUNGUA MKUTANI WA GAVI LEO

Tuesday, December 4, 2012

Na Heka Paul na Shakila Galus- MAELEZO- Dar es salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kufungua Mkutano wa Kimataifa wa wadau wa chanjo duniani (GAVI) utakaonza leo. Mkutano huo unatarajiwa kuwa washiriki 600 kutoka nchi mbalimbali duniani wakiwemo wake wa Marais , Mawaziri wa Afya, fedha na watu mashuhuri kutoka nchi 73. Kwa mujibu wa taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa jana mjini Dar es salaam na Kaimu Katibu Mkuu Regina Kikuli inasema kuwa lengo la mkutano huo ni pamoja na kujadili mafanikio na changamoto zinakabili huduma ya utoaji wa chanjo duniani. Taarifa hiyo inaongeza kuwa hii ni mara ya kwanza mkutano wa aina hiyo kufanyika Afrika mashariki na kuongeza kuwa sababu zilizopelekea mkutano kufanyika Tanzania ni pamoja na mafanikio makubwa katika utoaji wa huduma za chanjo za watoto na mama wajawazito. Hivyo basi washiriki watapata fursa ya kutembelea vituo vinavyotoa huduma za chanjo nchini ili kujionea mafanikio na changamoto zilizopo pamoja na kujifunza. Vilevile washiriki watapata fursa ya kujadili masuala ya chanjo ikiwemo uingizwaji wa chanjo mpya na masuala ya afya ya mama na mtoto. Pia kutakuwepo na uzinduzi wa chanjo mbili mpya za magonjwa ya kuhara, homa ya uti wa mgongo kwa watoto chini ya mwaka mmoja ambazo zinatolewa nchini kwa hisani GAVI.

0 comments:

Post a Comment