MKAZI wa Kijiji cha Kilombero, mkoani Geita, Mahangaiko Buruhe (52) amefariki dunia baada ya kusombwa na upepo mkali ulioambatana na mvua wakati akijaribu kuzuia nyumba yake isianguke. Tukio hilo lilitokea juzi saa 10;00 jioni ambapo marehemu alikuwa akizuia nyumba yake isisombwe na upepo baada ya kushuhudia paa la nyumba likiezuliwa na upepo. Marehemu aliamua kurukia kenchi ili kuzua nyumba isianguke kwa kutumia nguvu zake na kwamba upepo ulimzidi nguvu, paa likaezuliwa na marehemu kurushwa nje na kuangukia nyumba ya pili alikopoteza maisha. Mashuhuda wa tukio hilo Makwiwa Bihalale (mke wa marehemu) na Chausiku Malole walisema marehemu alikuwa akifanya juhudi za kuokoa nyumba isianguke na upepo ndipo mauti yakamkuta hali ambayo imewashtua. Akizungumza mbele ya viongozi waliotembelea hapo kuona tukio hilo, Kaimu Ofisa Tarafa ya Busanda, Joseph Kaparatus alisema tukio hilo lilitokana na ujenzi mbovu wa nyumba hiyo na kwamba iliezekwa bila kuzingatia utaalamu na haina kenchi zaidi ya mbao ambazo zimegongelewa bati. “Nyumba hii ilikuwa na uhalali wa kuanguka mkuu, angalia haijajengwa kwa kuzingatia utaalamu wa ujenzi wa nyumba,” alisema Kaparatus. Awali akizungumza na wakazi wa eneo hilo nyumbani kwa marehemu Mkuu wa Wilaya ya Geita, Said Mangochie aliwataka wanachi hao kujenga nyumba bora zinazozingatia utaalamu ili kuepusha majanga wakati wa mvua. Mwenyekiti wa kijiji hicho Haruna Shabani alisema marehemu aliwahi kuwa mtendaji wa kijiji, na kiongozi wa CCM Kata ya Busanda, ameacha wajane wawili na watoto 18.
Popular Posts
-
Rais wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Joseph Kabila amekanusha vikali madai kwamba alishinda uchaguzi wa nchi hiyo kupitia wizi wa kura...
-
Huduma ya Maji na Nishati (EWURA), Mhandisi Godwin Samwel, akizungumza na wanahabari jana jijini, Dar es Salaam kuhusu kupanda kwa bei za m...
-
Pope Benedict XVI is in the Spanish capital, Madrid, for four days of events expected to be attended by hundreds of thousands of people. ...
-
Mkesha ulofanyika katika uwanja wa Taifa wa mpira katika kuliombea Taifa
-
Waziri wa Usalama wa Nchi, George Saitoti, alisema jeshi litawasaka wafuasi wa kikundi cha waislamu wenye siasa kali, al Shabaab, kokote wa...
-
Maandamano kupinga uroho wa makampuni yamefanywa sehemu mbali mbali za dunia, yakitiwa moyo na maandamano ya wiki mbili sasa yanayofanywa N...
-
Katika kuitikia kaulimbiu ya kilimo kwanza Kampuni ya Utalii ya Cordial Tours Yenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam imeamua kuunga Mk...
-
ALIYEKUWA Mkurugenzi wa Utawala na Utumishi (DPA) wa Benki Kuu Tanzania (BoT), Amatus Liyumba ambaye anatumikia kifungo cha miaka miwili je...
-
MWANASIASA machachari ambaye pia ni Waziri wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, Samuel Sitta ametangaza nia ya kugombea Urais wa Jamhuri ya Mu...
-
Mwanamfalme wa Uingereza Charles na mkewe Camilla, au The Prince of Wales and The Duchess of Cornwall, kama wanavyojulikana rasmi, watafany...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)




0 comments:
Post a Comment