Taarifa kwa vyombo vya Habari * Vodacom na Nokia yaja na ofa ya funga mwaka * Maelfu ya zawadi kushindaniwa kwa wanunuzi wa simu za Nokia * Pia kufaidika na SMS, muda wa maongezi na internet za bure Dar es Salaam, Disemba 4, 2012 ... Wakati shamrashamra za maandalizi ya msimu wa sikukuu za mwishoni mwa mwaka yakiwa yanaendelea, Kampuni ya Vodacom Tanzania na Nokia zimetambulisha ofa kabambe kukamlisha furaha ya kuelekea kufunga mwaka wa 2012. Kampuni hizo kwa pamoja zimezindua rasmi shindano litakalomuwezesha mteja yeyote atakayenunua simu ya mkononi aina ya Nokia, kujishindia zawadi mbalimbali papo kwa hapo, pamoja na kupata fursa ya kuingia kwenye droo kuu. Mteja atakayenunua simu ya Nokia na kisha kuweka muda wa maongezi wa aidha Tsh 1,000 au Tsh 1,500 atapata kifurushi cha BURE chenye muda wa maongezi wa dakika 10, SMS 50 na internet ya MB10 kila siku kwa muda wa wiki moja. Kila simu ya Nokia itakayonunuliwa itakua na namba maalumu/kuponi ambayo mteja atatakiwa kutuma namba hiyo kwa SMS kwenda 15544 ili kuingizwa kwenye droo. Kila SMS itakayotumwa kwenda kwenye namba 15544 itatozwa gharama ya kawaida ya SMS. Washimdi wa droo hizo zitakazokuwa zikichezeshwa kila siku watakuwa wakijishindia zawadi za simu, chargers, t-shirts na headphones zitakazotolewa kwa wateja kama zawadi za papo hapo. "Ushiriki wa kubahatika kujishindia zawadi za papo hapo humuwezesha mteja kuingia moja kwa moja katika Droo kubwa ya mwisho itakayofanyika Januari 11, 2013 ambapo washindi watapata simu za kisasa za Nokia Lumia."Alisema Mkuu wa Udhamini na Mawasiliano wa Vodacom Kelvin Twissa Washindi wa zawadi za kila siku watachukua zawadi zao katika maduka ya Vodacom yaliyochaguliwa, ambapo watapatiwa huduma stahiki Shindano hilo litafikia tamati ifikapo Januari 10, 2013, majira ya usiku, na Januari 11, 2012 ndiyo siku ambayo Vodacom na Nokia zitachezesha droo itakayoshirikisha washiriki wote wa shindano hili toka mwanzo, na kati yao mshindi atatangazwa
Popular Posts
-
What to do in Zanzibar when you’re a tourist? I had booked myself a 4-day trip to the island, and, taking the advice of friends and a quic...
-
RAIS Jakaya Kikwete amewapandisha vyeo maofisa wakuu kutoka cheo cha Meja Jenerali kuwa Luteni Jenerali kuanzia Novemba 21,mwaka huu. K...
-
KUTOKANA na kile kichoonekana ni kutaka kukabiliana na uhaba wa sukari na kupanda kwa bei yake, Waziri Mkuu Mizengo Pinda anatarajia kukuta...
-
Na Heka Paul na Shakila Galus- MAELEZO- Dar es salaam Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Jakaya Mrisho Kikwete anatarajiwa kuf...
-
MBUNGE wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu Sugu, ameungana na wananchi wanaotaka Katiba Mpya ifute uwepo wa wakuu wa wilaya...
-
Brazil's government has said it will implement 50bn reais ($30bn; £19bn) of spending cuts in order to curb inflation and help prevent t...
-
The rankings of Africa’s top higher education institutions is provided by the 4 International Colleges & Universities (4icu). ...
-
Katika Teknolojia Wiki Hii - Polisi yawasaka watumiaji Blackberry, wadukuzi walenga Blackberry, mashine za kupaa zilizotengenezwa nyumbani ...
-
WAMILIKI wa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans jana walitoka mahakamani kwa furaha baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutupilia mba...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)
0 comments:
Post a Comment