JAJI Mkuu, Mohamed Chande Othman ameeleza sababu za kutokuwa kwenye jopo la majaji waliopangwa kusikiliza kesi ya aliyekuwa mbunge wa Chadema mkoani Arusha, Godbless Lema. Jaji mkuu, alitoa maelezo haya jana alipozungumza na gazeti hili katika mahojiano maalumu kwenye mahafali ya 12 ya Chuo cha Uongozi wa Mahakama Lushoto (IJA). “Ngoja nitolee ufafanuzi suala hilo ili jamii itambue utaratibu wa uendeshaji wa Mahakama ya Rufani, ambayo ina majaji 16 nchini,” alisema Jaji Othman. Jaji Othman alisema kimsingi hajajitoa kushughulikia kesi hiyo, ila siku ambayo kesi hiyo inatajwa, atakuwa nchini India kuhudhuria Mkutano Mkuu wa 13 wa Majaji Wakuu Duniani. Maelezo hayo ya Jaji Chande yamekuja siku tatu baada ya gazeti hili kuripoti kuwa, mkuu huyo wa mhimili wa Mahakama nchini amejitoa kusikiliza kesi hiyo na nafasi yake imechukuliwa na Jaji Bernard Luanda. “Kwanza ifahamike kwamba, jaji wa Mahakama ya rufani hana ubia na kesi yoyote kwa mujibu wa utaratibu. Jaji yeyote kati ya majaji 16 wa mahakama ya rufani nchini ana mamlaka ya kusikiliza kesi yoyote ya rufani,” alieleza Jaji Othman. Jaji Othman alifafanua kuwa, rufani ya Lema ni miongoni mwa kesi tatu za uchaguzi zilizobaki ambazo kwa mujibu wa taratibu za kisheria, huanza kusikilizwa baada ya muda wa mwaka mmoja na hukumu yake ni lazima itolewe ndani ya mwaka mmoja tangu kuanza kwake. “Hivyo basi, kwa vile Jaji yeyote wa Mahakama ya Rufaa anaweza kuisikiliza kesi hiyo, hakukuwa na sababu inisubiri mimi,” alisema. Jaji Othman alitaja kesi nyingine za uchaguzi zitakazoanza kufanyiwa vikao vya rufani na jopo la majaji wa Mahakama ya Rufani kuwa, ni ile ya Jimbo la Ubungo kati ya Hawa Ng’umbi na John Mnyika ambayo itakuwa chini ya jopo la majaji watatu; Jaji Nathalia Kimaro, Jaji Salum, Salum Masati na Jaji Katherine Oriyo. Nyingine ni ya Jimbo la Ilemela ya Yusuph Yussuph Masengela Lupilya na wenzake wawili dhidi ya Highness Kiwia na wenzake wawili, ambayo itakuwa chini ya jopo la Majaji Januari Msofe, Jaji Beard Luanda na Jaji Salum Massati. Alisema rufani ya Lema haijaanza kusikilizwa kwa jaji yeyote, hivyo yeye asingeweza kujitoa kwa kuwa hajapangiwa. “Kinachotatiza hapa ni kwamba, watu wanaifungamanisha rufani hii na ile ya Arusha ambayo mimi nilikuwa miongoni mwa jopo la majaji kama mwenyekiti.
Popular Posts
-
JAJI Mkuu, Mohamed Chande Othman ameeleza sababu za kutokuwa kwenye jopo la majaji waliopangwa kusikiliza kesi ya aliyekuwa mbunge wa Cha...
-
KIASI cha fidia ambacho Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco) liliamriwa na Mahakama Kuu Dar es Salaam, kuilipa Kampuni ya Kufua Umeme wa D...
-
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi (SACP) Liberatus Sabas akiwaonyesha waandishi wa habari (Ha...
-
Wazungu wawili raia wa Ujerumani, VEIXLAR MARLM (24), WEIXLER ROLAND (21) wamenusurika kuuawa baada ya kutekwa na watu waliojifanya waendes...
-
Nyaraka zilizonekana katika jengo la serikali ya Libya mjini Tripoli, zinaonesha uhusiano wa karibu baina ya mashirika ya ujasusi ya mataif...
-
Sheikh Mkuu wa Bakwata, Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kushoto), akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki katika Ma...
-
safara wa magari wenye ulinzi na silaha kutoka Libya umevuka mpaka kuingia nchini Niger, ripoti zinasema. Msafara huo unaaminika ni wa w...
-
Mtaalamu kutoka Finland asaidia mikakati ya tehama
-
MBUNGE wa Jimbo la Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi, maarufu Sugu, ameungana na wananchi wanaotaka Katiba Mpya ifute uwepo wa wakuu wa wilaya...
-
BAADA ya juzi Jeshi la Polisi kuwahoji na kuwaachulia huru wabunge wa Chadema, jana asubuhi walikamatwa na kutupwa korokoroni hadi kesho ...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)




0 comments:
Post a Comment