Saratani 'yamwuua Mugabe'

Wednesday, September 7, 2011


Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe ana saratani ya kibofu iliyoenea kwenye viungo vengine, kulingana na nyaraka za kidiplomasia za Marekani zilizofichuliwa.

Nyaraka hiyo, iliyochapishwa na mfichua siri Wikileaks, inamtaja gavana wa benki kuu Gideon Gono akisema daktari wa Mugabe amemsihi aachie madaraka.

Nyaraka hiyo, iliyoandikwa mwaka 2008 na ubalozi wa Marekani mjini Harare, pia inasema Bw Mugabe mwenye umri wa miaka 87 anaweza kufariki dunia ifikapo mwaka 2013.

Bw Gono, mshirika mwaminifu wa Bw Mugabe, amepuuzilia mbali nyaraka hizo akisema ni "taarifa za kubuni".

Nyaraka hizo zinamnukuu Bw Gono akisema saratani hiyo "imesambaa na, kulingana na madaktari, itasababisha kifo chake katika kipindi cha miaka mitatu mpaka mitano."

Katika mahojiano na shirika la habari la Reuters Septemba mwaka jana, Bw Mugabe- aliyekuwa madarakani tangu mwaka 1980- alipinga uvumi kuwa alikuwa akifa kutokana na saratani na alipooza.

0 comments:

Post a Comment