Wanasayansi wanasema mbu wanaoambukiza malaria wanaadimika katika sehemu za Afrika, lakini hawajui sababu.
Data kutoka nchi kama Tanzania, Eritrea, Rwanda, Kenya na Zambia inaonesha malaria inapungua haraka ; labda kwa sababu ya miradi kama ile ya kutumia vyandarua venye dawa.
Lakini wanasayansi wa Tanzania na Denmark wanasema hata mitego yao inanasa mbu wachache, kutoka elfu 5 mwaka wa 2004 na kushuka hadi mbu 14 mwaka wa 2009.
Mitego hiyo iko katika vijiji visivokuwa na vyandarua vya dawa.
Sababu inaweza kuwa mabadiliko ya hali ya hewa..kwamba misimu ya mvua imebadilika na hivo kuchafua msimu wa uzazi wa mbu.
Lakini aliyeongoza utafiti huo, Professor Dan Meyrowitsch, hakubaliani na hayo, anafikiri sababu hasa ni kuwa pengine kuna ugonjwa uliotapakaa kati ya mbu na kuwafyeka wengi, au mabadiliko katika mazingira yao ambayo hayawafai.
0 comments:
Post a Comment