Rais Jakaya Kikwete amesema nchi zilizo Kusini mwa Bara la Afrika zinatatizo kubwa la vyanzo vya mitaji hali inayoleta changamoto katika kukuza na kuendeleza uchumi wa nchi hizo.
Rais Kikwete ameyasema hayo wakati akichangia katika Mkutano wa Kimataifa wa Kibiashara wa Langkawi -LID ulioanza jana na unaotarajiwa kumalizika tarehe 23 mwezi huu nchini Malaysia ikiwa ni katika kutafuta nchi kushirikiana kibiashara ili kuinua uchumi wa nchi zinazoendelea.
Rais Kikwete amesema kwa upande wa Tanzania misaada inapatikana lakini haitosholezi mahitaji na masharti yake ni magumu hali inayoweza kuizamisha nchi kwenye mzigo mkubwa zaidi wa madeni na matatizo ambayo hayakutarajiwa.
0 comments:
Post a Comment