Sheikh Mkuu wa Bakwata, Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum (kushoto), akiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki katika Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW), Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam, usiku wa kuamkia leo. (Picha zote na Kassim Mbarouk-www.bayana.blogspot.
Baadhi ya waumini wanawake wakiwa kwenye hafla ya Maulid ya maadhimisho ya kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW), Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki (kulia), akimkaribisha Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi katika hafla hiyo ya Maulid.
Mbuge wa Ilala, Mussa Azzan Zungu, akiwa na baadhi ya viongozi wa Dini ya Kiislamu pamoja na wageni mbalimbali katika hafla hiyo.
Kikundi cha Ahbabi Rasulillah kikitumbuiza wakati wa Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW), Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo kwa ala tupu.
Kikundi cha Ahbabi Rasulillah kikitumbuiza wakati wa Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW), Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo kwa ala tupu.Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto), akiwa na Mwenyekiti wa kampuni za IPP, Reginald Mengi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki na Kamnda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, wakiitikia dua iliyokuwa ikiombwa na Sheikh Sharif Hussein Badani (kushoto), kutoka nchini Kenya, wakati wa Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW), Viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi (wa pili kushoto), akiwa na Mwenyekiti wa kampuni za IPP, Reginald Mengi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Saidi Sadiki na Kamnda wa Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, wakiitikia dua iliyokuwa ikiombwa na Sheikh Sharif Hussein Badani (kushoto), kutoka nchini Kenya, wakati wa Maulid hayo.
Ustaadhi Imadi Rabbi kutoka Misri akisoma Kur'an, wakati wa ufunguzi wa Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW), Viwanja vya Mnazi Mmoja. Kulia ni Sheikh wa Bakwata Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salim.
Ustaadhi Imadi Rabbi kutoka Misri akisoma Kur'an, wakati wa ufunguzi wa Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa Mtume Muhammad (SAW), Viwanja vya Mnazi Mmoja.
\Kikundi cha Ahbabi Rasulillah kikitumbuiza wakati wa Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW), Viwanja vya Mnazi Mmoja kwa kaswida inayojulikana kwa jina la Bado hujachelewa, Dar es Salaam usiku wa kuamkia leo.
Sheikh Mkuu wa Bakwata, Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salim, akitoa salamu zake za Maulid wakati wa maadhimidho hayo, usiku wa kuamkia leo, Viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Imamu Mkuu wa Msikiti wa Buguruni Kwamnyamani, Sheikh Idd Muhammad Idd, akiwa na Mbunge Profesa Kapuya, kwenye maadhimisho hayo.
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akimkabidhi picha Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini, Murtaza Sabouri (kulia), kutokana na Baraza la Kiislamu Tanzania (Bakwata), Mkoa wa Dar es Salaam, kutambua mchango wake katika kupatanisha na kuwaunganisha watu wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini, wakati wa maadhimisho hayo.
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akimkabidhi picha Mkurugenzi wa Kituo cha Utamaduni cha Iran nchini, Murtaza Sabouri (kulia), kutokana na Baraza la Kiislamu Tanzania (Bakwata), Mkoa wa Dar es Salaam, kutambua mchango wake katika kupatanisha na kuwaunganisha watu wa madhehebu mbalimbali ya dini nchini, wakati wa maadhimisho hayo.
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akizungumza katika hafla ya maadhimisho hayo.
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akiagana na baadhi ya waumini wa Dini ya Kiislamu, mara baada ya kusimama Kiamu kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad.
Mmoja wa wasomaji wa Maulid hayo, akisoma mlango wa Sita (Kiamu) katika kuadhimisha kuzaliwa kwa Mtume Muhammad (SAW), viwanjani hapo.
Rais mstaafu wa Awamu ya Pili, Alhaj Ali Hassan Mwinyi, akiwa katika kisimamo katika maadhimisho hayo.
Baadhi ya viongozi wa dini, Taasisi, Wabunge na wageni mbalimbali wakiwa katika kisimamo cha Maulid ya kuadhimisha kuzaliwa Mtume Muhammad viwanjani hapo usiku wa kuamkia leo.
Mwenyekiti wa Chama cha NCCR Mageuzi, Joseph Mbatia akizungumza na waandishi wa habari, wakati wa hafla ya maadhimisho hayo.
Chini na juu wakundi vya Dufu vikitumbuiza kwa kaswida mbalimbali wakati wa maadhimisho hayo, usiku wa kuamkia leo.
Rais Kikwete amtembelea Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour Jumaa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na Rais mstaafu wa Zanzibar, Dk. Salmin Amour Jumaa, alipomtembelea kumjulia hali nyumbani kwake Zanzibar Jumatatu Januari 13, 2014 baada ya
kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya Mapinduzi.
This is nice topic where people has to go through