Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe wa tatu kulia akiwa na mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Solomon Madaha wa tatu kulia ,mwenyekiti wa CCM wilaya ya Ludewa Bw Kolimba na viongozi wengine wakitembelea ziwa nyasa
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjome wa pili kushoto akimwonyesha mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha kushoto nchi ya Malawi inavyoonekana ukiwa eneo la Manda mwambao mwa ziwa Nyasa baada ya kutembelea eneo hilo kuhamasisha wananchi kuendelea na shughuli zao na kuondoa hofu ya kutokea vita ya mpaka kati ya nchi ya Malawi na Tanzani.a.
Na Francis Godwi Blogu Ludewa
MBUNGE wa jimbo la Ludewa mkoani Njombe Deo Filikunjombe amepongeza jitihada kubwa zilizofanywa na serikali ya chama cha mapinduzi (CCM) chini ya Rais Dr Jakaya Kikwete katika kumaliza mgogoro wa mpaka kati ya Tanzania na Malawi na kuwataka wananchi wanaoishi mwambao wa ziwa Nyasa kuendelea na shughuli zao bila hofu yoyote.
Filikunjombe alisema kuwa serikali ya Rais Kikwete ni serikali sikivu na ndio sababu ya kulishughulikia suala hilo la mgogoro wa mpaka kwa wakati zaidi bila kutokea machafuko ya aina yoyote .
Akizungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa kata ya Ilela na Manda wakati wa ziara yake ya kusherekea pamoja na wapiga kura wake sikukuu ya Krismas na Mwaka mpya juzi ,Filikunjombe alisema kuwa awali baada ya kuwepo kwa taarifa ya Rais wa Malawi Joyce Banda kudai ziwa Nyasa lote ni mali ya nchi yake ya Malawi wananchi wa Tanzania wanaoishi jirani na ziwa hilo upande wa Tanzania walianza kuigiwa a hofu kubwa .
Mbali ya kuingiwa na hofu hiyo ya kiusalama ila bado walikuwa wakifanya shughuli zao kwa hofu kubwa na baadhi yao kushindwa kuwajibika vema katika shughuli za kimaendeleo kwa kuhofu vita kutokea .
Hata hivyo alisema kutokana na serikali ya CCM kuwa sikivu zaidi baada ya kubaini suala hilo mara moja jitihada za kulifanyia kazi hilo bila kumwaga damu ilianza kufanyika na kuwa kwa sasa Rais Kikwete amemaliza mgogoro huo na hakuna tatizo tena.
” Ninawahakikishia wananchi wangu wa Manda na Ilela pamoja na kata nyingine zote kama Makonde, Lifuma na zote ambazo zipo jirani na ziwa Nyasa na wanategemea maisha yao kwa kuvua samaki na dagaa katika ziwa hilo ….kuendelea na shughuli zao bila hofu yoyote” alisema mbunge Filikunjombe huku akishangiliwa na wananchi hao
Alisema kuwa Rais Kikwete amekuwa akijituma sana katika kuwatumikia watanzania ila wapo baadhi ya watendaji wa serikali ambao ni mzigo katika serikali yake na wamekuwa wakishindwa kuwatumikia wananchi vema.
Filikunjombe alisema yeye kama mbunge na mwakilishi wa wananchi wa jimbo la Ludewa kamwe hatakubali kuona wananchi wake wanakosa huduma za msingi kama ilani ya CCM inavyosema kutokana na baadhi ya viongozi kushindwa kutimiza majukumu yao vema.
Alisema kuwa kwa kutumia fursa za ziwa Nyasa wananchi wa maeneo ya mwambao mwa ziwa hilo wanaweza kujikwamua kiuchumi kwa kupatiwa vitendea kazi vya kisasa kwa ajili ya uvuvi badala ya kuendelea kuifanya kazi hiyo kwa kutumia vitendea kazi duni na kufanya uvuvi wao kutokuwa na tija ya kimaendeleo.
Akizungumza kwa niaba ya wananchi wenzake John Haule alisema kuwa awali walikuwa na hofu kubwa ya kuendelea kufanya shughuli za maendeleo kutokana na hofu ya kutokea vita ya mpaka kati ya Malawi na Tanzania na kuwa hata wakati mwingine wakiona ndege zikipita angani walikuwa wakiogopa kuwa yawezekana ni ndege za vita kutoka Malawi na zinataka kuwaangamiza.
“Tunakupongeza kwanza wewe mwenyewe mbunge wetu Deo Filikunjombe kwa kutuwakilisha vema kwa Rais Kikwete na bungeni pia tunataka kuwaeleza viongozi wa CCM sisi wana Ludewa tumechoka kuendelea kuwa na mbunge wa kipindi kimoja kimoja sisi kwa sasa hatuhitaji mbunge mwingine zaidi yako na kama watafanya wao watakavyo tupo tayari kuhama na wewe papote”
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Ludewa Juma Madaha mbali ya kuungana na mbunge Filikunjombe kuwahakikishia usalama wananchi hao bado alisema kuwa ni vema wananchi hao kutumia mvua zilizopo kwa kulima mazao yanayohimili ukame kama mihogo ambayo imekuwa ikistawi zaidi katika maeneo hayo .
Kwani alisema kuwa wataalam wa hari ya hewa wanadai kuwa hali ya mvua kwa mwaka huu si nzuri sana pia upo uwezekano wa mwakani Taifa kutokuwa na neema kutokana na wataalam hao katika uzoefu wao kuonyesha miaka yote inayo malizika na namba 4 kuwa na tatizo la neema.
0 comments:
Post a Comment