UPELELEZI wa kesi inayomkabili Msanii wa filamu nchini, Elizabeth Michael maarufu kama Lulu, anayekabiliwa na kesi ya mauaji katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, bado haujakamilika. Hayo yalielezwa jana na Wakili wa Serikali, Keneth Sekwao wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa na kuangalia kama upelelezi utakuwa umekamilika au la. Sekwao alidai mahakamani hapo kuwa, upelelezi haujakamilika na kuomba ipangiwe tarehe nyingine kwa ajili ya kutajwa. Baada ya kutolewa kwa maelezo hayo, Hakimu Mmbando aliiahirisha kesi hiyo hadi Desemba 17, mwaka huu. Lulu anatuhumiwa kumuua msanii mwenzake, Steven Kanumba. Anadaiwa kutenda kosa hilo Aprili 7, 2012 nyumbani kwa marehemu, Sinza Dar es Salaam. Hata hivyo, umri wake ulizua mvutano mkali baina ya upande wa mashtaka katika kesi hiyo na jopo la mawakili wanaomtetea, mvutano ambao ulianzia Mahakama ya Kisutu na kuendelea hadi Mahakama ya Rufani, huku kesi ya msingi ikiwa haijaanza kusikilizwa. Juni 11, mwaka huu Mahakama Kuu ilikubali kufanya uchunguzi wa umri halali wa mshtakiwa, kufuatia maombi yaliyowasilishwa mahakamani hapo na jopo la mawakili wanaomtetea Lulu. Upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Elizabeth Kaganda, akisaidiana na Wakili wa Serikali, Shadrack Kimaro waliwasilisha maombi Mahakama ya Rufani wakiomba ifanye marejeo ya uamuzi wa Mahakama Kuu, kama ulikuwa sahihi. Jopo la majaji watatu wa Mahakama ya Rufani lililoongozwa na January Msoffe, Jaji Bernard Luanda na Edward Rutakangwa, lilizima mvutano na likaamuru kuendelea kwa kesi ya msingi. Katika uamuzi uliosomwa na Naibu Msajili wa Mahakama ya Rufani, Zahra Maruma, jopo hilo kwanza lilisema maombi ya marejeo ya uamuzi wa Mahakama Kuu, yaliyowasilishwa na Jamhuri yalikuwa batili.
Popular Posts
-
WIZARA ya Nishati na Madini, imesema tatizo la umeme nchini linatokana na kuchoka kwa miundombinu na hivyo kuzidiwa nguvu. Kauli hiyo ...
-
What to do in Zanzibar when you’re a tourist? I had booked myself a 4-day trip to the island, and, taking the advice of friends and a quic...
-
SERIKALI itatoa leseni kwa wafanyabiashara wa hapa nchini, ili kuwawezesha kuagiza tani 120,000 za sukari kutoka nje ya nchi na sukari hiyo...
-
Rap icon Tupac Shakur covers the latest issue of XXL in a profile that celebrates the rapper, who passed away 15 years ago. In the latest...
-
BAADHI ya wananchi wa Ubungo katika Manispaa ya Kinondoni, jana wavamia Ofisi za Kampuni inayosambaza maji katika Jiji la Dar es Salaam na...
-
WAMILIKI wa Kampuni ya kufua umeme wa dharura ya Dowans jana walitoka mahakamani kwa furaha baada ya Mahakama Kuu ya Tanzania kutupilia mba...
-
Chimbuko la uvujaji wa mitihani nchini Tanzania lina historia ndefu inayoenda sambamba na kuundwa kwa BARAZA LA MITIHANI LA TAI...
-
RAIS wa Uganda, Yoweri Museveni amewapandisha vyeo maofisa wa juu wa jeshi pamoja na kuwahamisha baadhi ya maofisa akiwemo mlinzi wake mk...
-
I: UTANGULIZI a) Masuala ya Jumla Mheshimiwa Spika, 1. Ni jambo la kumshukuru Mwenyezi M...
-
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania DK.Jakaya kikwete akilihutubia bunge mjini Dodoma.kulia ni spika wa Bunge Anne Makinda. Wab...
Habari Leo Tanzania, Media, (East Africa)




0 comments:
Post a Comment