Katika kuitikia kaulimbiu ya kilimo kwanza Kampuni ya Utalii ya Cordial Tours Yenye makao makuu yake Jijini Dar es salaam imeamua kuunga Mkono kauli mbiu ya serikali kwa kuandaa safari ya utalii katika masuala ya kilimo ambapo timu ya wakulima kutoka mikoa mbalimbali wameenda nchini Israel kushiriki maonyesho ya kimataifa yanayohusu ukulima wa kisasa pamoja na kujifunza ikiwepo kuwaunganisha na wakulima wakubwa Duniani ili waweze kuja kuwekeza hapa nchini katika sekta ya kilimo ambayo ndiyo inaweza kulikomboa taifa hili kiuchumi.
Katika mahojinao maalumu na Gazeti hili Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo hapa nchini Bw.David Kizito alisema Kampuni yake imejipanga kuhakikisha Watanzania wanaielewa vyema sera ya Serikali ya Kilimo kwanza na sisi kama kampuni tumeamua kuinga mkono serikali kwa vitendo kwa kuratibu safari za mafunzo kwa wenzetu Waisrael ambao wamefanikiwa sana katika eneo la Kilimo na kuwaunganisha wakulima na wawekezaji wakubwa kutoka Israel.
Mbali na kuratibu safari za mafunzo pia tunatafuta uwezekano wa kuanzisha mafunzo kwa walima nchini kote na mipango inaendelea ili ikiwezekana tuweze kujenga chuo cha kilimo watu waweze kujifunza na hatimaye tuweze kubadilisha kilimo chetu kuwa cha kisasa.
Mtaalamu mmoja kutoka Israel aliwahi kuniambia kuwa Tanzania ni nchi tajiri sana kwani Dodoma pekee yake kabla hujaenda maeneo mengine ina uwezo wa kulisha Afrika nzima na kama Tanzania itaweka kipaumbele kwenye kilimo upo uwezekano kwa Taifa hili kuilisha Dunia kwani Israel ni jangwa lakini walipotia bidii katika mageuzi ya kilimo cha kisasa leo hii Taifa lao linalisha karibu nusu ya dunia na uchumi wao umepiga hatua kwa kuuza mazao kwa wingi katika soko la Dunia.
Akifafanua zaidi alisema katika safari ya kwanza ya kwenda kujifunza watanzania wakuwa Israel kwa muda wa siku saba na watashiriki katika maonyesho ya kilimo kutoka mataifa mbalimbali na watakwenda kutembelea mashamba ili waone kwa vitendo pamoja na kuwaunganisha na wakulima wakubwa ili waweze kuona namna ya kuja kuwekeza katika medani ya kilimo.
Kutokana na wananchi wengi kuhamasika kwenda kujifunza Kampuni yake imeamua kuandaa safari nyingine ya mafunzo nchini Israel ambayo itakuwa tarehe 8-18 februaly 2014 na hii ni kuitikia maombi kutoka kwa wananchi wengi ambao wameiomba kampuni kuandaa safari nyingine kwani katika safari hii ya maonyesho tulipewa nafasi 20 tu lakini safari ijayo tuna nafasi zaidi ya 200 ambazo tumepewa.
Nitumie fursa hii kuwaomba watanzania kujiandikisha kwaajili ya safari ya mwezi ujao kwani mafunzo ndio njia pekee inayoweza kugeuza uchumi wetu kwa kupitia sekta ya kilimo na si vinginevyo.
Mwandishi wa makala hii anapatikana kwa simu0752930541.smnoza@yahoo.com.
0 comments:
Post a Comment