Marekani imo katika shughuli za kuwakumbuka waliokufa katika mashambulio ya Septemba 11, miaka 10 iliyopita, katika miji ya Washington na Pennsylvania.
Kuna ulinzi mkali, kufuatia onyo kwamba huenda kundi la magaidi la al-Qaeda likafanya mashambulizi.
Jamaa za waliokufa katika mashambulio ambako ndege nne zilizokuwa zimetekwa na magaidi zilishambulia majumba, na kusababisha vifo vya karibu watu 3,000.
Kwa kila ndege iliyohusika katika shambulio, watu walinyamaza kimya kwa dakika moja.
Waombolezaji, waliingia kwa foleni katika eneo la Ground Zero, na ambalo lina majina ya wote waliokufa katika mashambulio hayo.
Majini hayo yalisomwa wakati wa shughuli hiyo, huku wengi wakishindwa kuvumilia, na kutiririkwa na machozi.
Rais wa Marekani Barack Obama alisoma aya za Biblia, Zabur 46, katika shughuli hizo mjini New York.
"Mungu kwetu sisi ni kimbilio na nguvu, msaada utakaoonekana tele wakati wa mateso. Kwa hiyo hatutaogopa itakapobadilika nchi, Itakapotetemeka milima katikati mwa bahari ", alisoma Rais Obama.
Aliandamana na mkewe, Michelle, hadi Pennsylvania, ambako waliweka shahada katika uwanja mmoja wa kumbukumbu, Shanksville, ambako ndege moja ilianguka baada ya abiria kupambana na magaidi walioiteka ndege hiyo.
Kuna ukumbusho mwingine mahali ambapo majengo ya World Trade Centre yalikuwepo.
Vifaa vya kukagua vitu vya chuma vinatumika katika juhudi za polisi za kuwakagua watu wanaofika mahali palikuwepo majengo ya World Trade Centre, huku maafisa wa polisi New York na Washington wakisimamisha magari yanayopita njia za chini kwa chini na daraja katika miji hiyo.
Shirika la Marekani la ujasusi, CIA, wiki iliyopita lilipata habari kwamba huenda kundi la al-Qaeda likawatuma watu kuwashambulia raia wa Marekani, au kuulipua mji mmoja kati ya miji mingi ya Marekani.
0 comments:
Post a Comment